Seth Bosco Hana Mpango Wa Kumuona Lulu

Mdogo wa aliyekuwa msanii wa bongo movies Steven Kanumba  ambae hivi sasa na yeye pia ameingia katika tasnia ya movies anaejulikana kama Seth Bosco amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana mpango wa kwenda gerezani kumuona Lulu Michael amabe alikuwa shemeji yake kwa kaka yake lakini pia alikuwepo siku ya tukio ya kuuawa kwa kaka yake huyo.

Seth alisema kuwa kwa sasa amekuwa na kazi nyini sana kwaiyo hawezi kwenda  kumuona Lulu akipata muda siku nyingine ataenda tu kumuona kwa sababu Lulu yupo tu siku yoyote  ataenda kumsalimia.

Sina mpango na sijapanga kabisa kwenda kumuona maana nina kazi nyingi sana na zinanibana sana, hivyo muda wangu ni mdogo sana, nina kazi nyingi sana za watu, lulu yupo tu nitaenda kuuona siku yoyote.Alisema Seth mdogo wake Kanumba.

Lulu Michael ambae alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mapema Novemba hii baada ya kukutwa na hatia ya kumuua  marehemu steven kanumba ambae alikuwa mpenzi wake bila kukusudia  alianza kutumikia kifungo hicho  mara baada tu ya kusomewa kifungo hicho  mahakamani hapo na kukataza ndugu zake kufuatilia kitu chochote kuhusu rufaa kwa sababu alisharidhika na hukumu hiyo..

Hata hivyo ndugu wa marehemu kanumba akiwepo mama na baba yake walikuwa ni moja ya watu waliolalamikia sana hukumu ya lulu na kusema kuwa hukumu hiyo haiendani na kile alichokifanya Lulu Elizabeth Michael. Baba mzazi wa Kanumba alisema kuwa hukumu hiyo inafanana na hukumu ya muua kuku.

Kanumba alikuwa katika mgogoro wa kimapenzi na mwandani wake huyo alipokuwa nyumbani kwake Sinza usiku wa tarehe 4 April mwaka 2o12, na kuanguka chini na kupoteza fahamu, lakini hata baada ya kwenda hospitali na kupatiwa huduma alikutwa tayari ameshakufa.

Mdogo wa Kanumba Atoa Ushahidi Kesi Ya Lulu

Ikiwa ni kama muendelezo wa kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya mfalme wa bongo moves Steven Kanumba, kesi inayomkabili aliyekuwa mpenzi wake ambae pia kwa sasa ni malkia wa bongo movies na amekuwa akifanya vizuri sana katika kazi yake Elizabeth Lulu Michael, shaidi wa kwanza ametoa ushahidi wake oktoba 19 kuhusu alichokuwa anakijua kuhusu mauaji hayo.

Seth Bosco ambae ni ndugu wa marehemu kanumba alitoa ushahidi wa kile kilichotokea katika kifo hicho miaka mitando iliyopita, akitoa ushahidi huo mbele ya mahakama, Seth Bosco alisema kuwa siku ya tukio la kifo cha Kanumba wawili hao walikuwa na mgogoro ambao ulisababishwa na msanii Lulu Michael kuongea na simu na na simu hiyo ilisadikika kuwa ni ya mwanaume mwingine.

Mbali na Seth Bosco, kulikuwa na shahidi mwingine ambae ni daktari aliepokea mwili wa marehemu ambae siku ya jana hakuweza kufika kutokana na hudhuru ya kuumwa, hata hivyo shahidi huyo anatarajiwa kufika mahakamani kwa ajili ya ushahidi siku inayofuta ya tarehe 20.

Baadhi ya watu walihudhuria mahakamani hapo ni pamoja na Muna akiwa kama rafiki wa karibu wa familia ya Lulu Michael,Dk.Cheni, mama mzazi wa Elizabeth Lulu Michael ,a mama mzazzi wa Kanumba ambae muda wote alionekana kuwa ni mtu  hasiye na furaha.

Steven Kanumba na Elizabeth Michael walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ,Kanumba alifariki April 2012 baada ya kuanguka kulikosadikika kulisababishwa na ugomvi  aliokuwa nao na mpenzi wake huyo.Hata hivyo ksi hiyo inayomkabili Lulu Michael ni kesi ya kuua bila kukusudia.Kesi ya Lulu itaendelea leo tarehe 20 Oktoba 2017.

Mungu awatie moyo familia zote zinazohusika katika kesi hii.

Elizabeth Michael  akiwa mahakamani