Snura Afunguka Kupewa Mimba na Kibenten

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Snura Mushi maarufu kama Snu Sexy amefunguka na kuongelea Mahusiano Yake na mpenzi wake ambaye pia ni msanii mwenzake maarufu kama Minu Calypto.

Kwa Miezi kadhaa sasa kumekuwa na taarifa kwamba Snura ni mjamzito na Baba wa mtoto huyo sio mwingine bali ni kibenten cha Snura.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Snura amefungukia Mahusiano Yake na kijana huyo na kuweka wazi kuwa wana mahusiano na kuhusu ujauzito amewataka watu wasubiri wajionee:

Tusubiri tu muda utafika tutaiona kama kweli ipo au haipo, maana mimba huwa hazijifichi itajulikana tu.

Mimi mwenyewe huwa nashangaaga watu wanadai eti natoka na kibenten, kwa sababu mimi sio mtu wa kwanza kufanya hivyo hata mtume wangu Mohammed (SW) alizidiwa umri na mkewe. Alimzidi karibia miaka 15 kwa hiyo hilo suala sio mimi wa kwanza kulianzisha sisi wenyewe tumelikuta kwa hiyo sio kitu cha ajabu.

Snura ambaye tayari ni mama wa watoto wawili alitengeneza sana headlines baada ya kujulikana kuwa ana uhusiano na Minu ambaye ni kijana mwenye umri mdogo sana kwake.

Msanii Snura Mushi na Mpenzi Wake Wapata Ajali Ya Gari

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko ya Mduara Snura Mushi ‘Snu Sexy’ pamoja na mpenzi wake Minu Calypto wamepata ajali ya gari siku ya jana mkoani Lindi walipokuwa anaelekea Kwenye shoo.

Taarifa za awali zinadai kuwa ajali hiyo ilitokea wakati Dereva wa gari la Snura alipokuwa anajaribu kulikwepa korongo na kusababisha gari hilo kupinduka.

Ndani ya gari hilo kulikuwa kuna watu watatno ambao ni Snura na Minu pamoja na madancer wawili wa Snura pamoja na Dereva wa gari hilo lakini kwa bahati nzuri kila mtu ni mzima zaidi ya majeraha machache.

Mpenzi wa Snura ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu ajali hiyo:

https://www.instagram.com/p/BmRRmsnFpXz/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=rzkvn5quub6p

Nisha Amponda Bwana wa Snura Adai ni Kiben-10 Kula Kulala

Muigizaji  wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu mtandaoni Nisha Bebe amewatolea povu wanaume wote wanaopenda kulelewa na wamama watu wazima ambao wanajulikana kama viben-10 au Marioo au Serengeti boys.

Wiki chache zilizopita kuna stori ilitrend mtandaoni kuwa Nisha kaporwa kiben-10 chake na msanii wa Bongo fleva Snura Majanga. Kijana huyo anayejulikana kama Minu Calypto alikuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Nisha kwa mara ya kwanza ambaye alikuwa na umri mdogo kuliko yeye.

Minu hivi sasa kajiweka kwa mwanamke ambaye ni wazi kuwa ni mkubwa kuliko yeye maana Snura anaonekana kama mtu mzima kwa Minu. Baada ya picha za Minu na Snura kusambaa siku ya Valentine’s Day na kuthibitisha uhusiano wao, Nisha amewatolea povu zito viben-10

Kupitia kipindi cha FNL ya East Africa Tv, Nisha amemtolea povu aliyekuwa bwana ale Minu na kumuita kula kulala ambapo aliwaandikia:

Mnazingua kwaiyo mnadhani mimi naweza kutiwa stress na mwanaume kula kulala?nimeanza kusafiri tangu 2013 now ni 2018, Niacheni jamani tafadhali”.

Nisha amesema hawezi kukaa na kuumia kisa mwanaume ambaye alikuwa hamsaidii kitu chochote maishani mwake.