Nisha Bebe Akana Tuhuma Za Kumiliki Kibenteni Kipya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nisha Rajabu ameibuka na kutolea povu Tetesi za kutoka kimapenzi na kijana ambaye amemzidi umri               (Kibenteni).

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Nisha Bebe amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa kwa sasa yupo mapenzini na mtu ambaye asingetamani kumuweka wazi na amemzidi umri na kwa upande wa Watanzania ameshamalizana nao.

Kuna kitu wacha nikiweke sawa, kuna post niliona kama sio jana basi juzi inasambaa kunihusu sijui nna kiben ten mpya sijui nini na nini.Wapendwa huko me nimeshavuka tangu 2016,nilishaapa kutokudate na mtu niliyemzidi umri pamoja na kipato,na kudate Mtanzania mwenzangu kwangu ni mwiko tena”.

Wakatimwingine tunakaa kimya kutokana na kuona kujibu jibu ni utoto,niko kwenye miaka ambayo hatudhungumzi sana,hatuna show off,tunaishi maisha yetu na tunapunguza mambo mengi ambayo siyo ya msingi”.

https://www.instagram.com/p/BsS2bNLA13A/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1g3lrkoj7s6py

 

Nisha Amfanyia MwanayeBonge La Party Nchini China

Muigizaji wa Bongo movie na Msanii wa Bongo fleva Salma Jabu maarufu Kama Nisha amekiri kumfanyia bonge la party nchini China binti yake mwenye umri a miaka 14.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nisha amekiri kumfanyia party hiyo binti yake  huyo anayeitwa Ipsum kwa sababu ndiye kila kitu kwake kwani anaye huyo pekee hivyo anamfanyia kile kitu kinachomfurahisha maishani mwake ili afurahie uwepo wake.

Mwanangu nimemfanyia sherehe ya bethidei China ambayo imegharimu milioni nane, tumekuja kufanya huku maana ndipo alipopachagua nami kwa kuwa nampenda na ndiye mwanangu wa pekee nikamleta na amefurahi sana na anajivunia kuwa na mama kama mimi pia nafurahi kuwa na mtoto mkubwa hivi kwa sasa“.

Mastaa wengi wameonekana kwenda nje ya nchi na watoto wao na kufanya mambo ya kufuru ambapo Wiki chache zilizopita Aunty Ezekiel na yeye alimbeba binti yake Cookie na kwenda kufanya naye bonge la party nchini Dubai.

Siri ya Mahusiano ya Mzungu na Nisha Yafichuka.

Hivi karibuni mwanadada Nisha alikuwa akiweka picha na video katika ukurasa wake wa instagram na hata alipohojiwa alisema kuwa kwa sasa ameamua kutoka katika mahusiano na vijana weusi na kuamua kuingia katika mahusiano na wazungu akiamini kuwa hao watakuwa na mapenzi ya kweli na sio vinginevyo.

Lakini baada ya muda mfupi ilitoka video ilimuonyesha nisha ambae kwa sasa ameamua kujiingiza katika sanaa  ya muziki akiwa  na mzungu huyo kama video model wake.lakini hiyo haitoshi kusema kuwa waili hao sio wapenzi hivyo baadhi ya magazeti yaudaku yakianza kufukunyua kuhsusu undani wa mzungu huyo.

Kwa bahati nzuri alipatikana mwanamke wa mzungu huyo ambae hapo awali alilalamika kuibiwa mume wake lakini sasa hivi anaonekana yupo sawa baada ya kupata ufafanuzi wa kile alichokuwa akikifanya mume wake.

Mwanadada huyo aliejitambulisha kwa jina la Felister anasema kuwa nisha alikuja nyumbani kwao na kumuomba mme wake ili waende kushoot video ambapo hata zile picha zilikuwa zipo katika huo wmbo lakini haikuwa makubaliano yao kuwa akatangaze kuwa yuke ndio mwanaume wake.

Kwa kumalizia mwanadada huyo alisema kuwa kwa sasa walishaongea na wameyamaliza na kila kitu kipo sawa.

 

Nisha Aamisha Majeshi Yake kwa Mzungu.

Msanii wa bongo movie Nisha amefunguka na kusema kwa sasa ameamua kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mzungu na sio waafrika tena na vibenten kama hapo awali  na kusema kuwa kwa sasa mapenzi yake yatakuwa na wanaume  waliomzidi umri yaani babu kwa sababu amechka maswala ya kuibiwa mabwana kila siku.

Katika ukurasa wake wa instagram, nisha ameweka picha na kuelezea kuwa amechoshwa sana na kuwa mhangawa mapenzi kila siku lakini anaamini hapo atakuwa salama na hatoibiwa wala kushalilishwa kwa matuzi kama alivyokuwa akifanyiwa na vijana wadogo.

ni vigumu sana kuficha hisia zangu kwa mtu ninayempenda, nimeshwahi kuwa na m-black, mwarabu,ila kote niliambulia usaliti na uongo katika mapenzi.niliwahi kusikia wazungu wana mapenzi ya kweli kuliko waafrika na kujaribu sio mbaya.

Mimi msafiri sijafika bado na mwenyezi mungu ndio anaejua kama hapa ndio mwisho wa safari yangu au bado ninaendelea,kikubwa nimeshampata na maneno sijali.

Hapo awali nsiha alikuwa akilizwa sana na mapenzi kutokana na kuibiwa na wanaume kila siku na wengi wao walikuwa ni wanaume aliowazidi umri ‘kibenten’ hivyo kwa maoni yake anaona sasa hivi atatulia.

Kibenteni Kilinigeuza Mimi ‘ATM’ Yake – Nisha

Muigizaji wa Bongo movie ambaye hivi karibuni amegeukia tasnia ya Bongo fleva na kuachia wimbo wake unaojulikana kama ‘Bachela’ amefunguka jinsi kibenteni chake kilivyokuwa kinamchuna.

Nisha amefunguka na kuelezea jinsi alivyowahi kuteswa na penzi la kijana mwenye umri mdogo kuliko yeye kwani ilibidi yeye ndio awe anampa huduma zote kijana yule.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nisha amesema kuwa wakati akiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na kibenteni huyo ambaye hakutaka kumtaja jina alikuwa akimnunulia kila kitu na kumpa fedha na kumuhudumia kama mtoto wake lakini baadaye alikuja kushtuka kuwa anachunwa na kua­mua kuachana naye.

Nimejifunza sana na nime­koma kuwa na uhusiano na mwanaume ninayemzidi umri na kipato maana nilijikuta nime­ingia kwenye uhusiano huo bila kujua kwamba kibenteni huyo ni tege­mezi ambaye alinifanya kama mashine yake ya ATM na kuniko­moa kuja kushtuka ameshanikwan­gua vya kutosha”.

Nisha ingawa amekiri kuwa mara ya kwanza wakati anaanza mapenzi na kijana huyo hakujua kuwa ni mdogo lakini baada alimpenda na kuendelea naye jambo ambalo anajutia kupita kiasi.

 

Nisha- Najutia Kuwa Kwenye Mahusiano Ya Kimapenzi na Viben 10

Muigizaji wa Bongo movie ambaye hivi karibuni amegeukia tasnia ya Bongo fleva, Nisha Bebe amefunguka na kukiri kuwa alishawahi kuwa na kiben 10.

Siku ya jana kuna video ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Nisha akiwa anahesabu pesa huku akisema kuwa tangu ameacha tabia ya kulea viben10 amekuwa na pesa nyingi.

Nisha amekiri kuwa alishawahi kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na kijana ambaye alikuwa amemzidi umri lakini amesema mara ya kwanza alipoanza naye Mahusiano hakujua hilo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Nisha amefunguka haya kuhusu ishu hiyo:

Nimeshawahi kuwa Kwenye Mahusiano na mwanaume ambaye nimemzidi umri na ikitokea kwamba tulivyokutana sikufahamu kwamba nimemzidi umri lakini baada ya kuwa pamoja na kujuana zaidi ndio nikajua nimempita miaka kadhaa.

Lakini pia nimeshawahi kujutia kuwa na mwanaume ambaye nimemzidi umri   kwa  sababu mimi ndio nilikuwa kama namuhudumia kwa kila kitu na zaidi nilipoteza tu muda na nimejutia sana sana sana “.

Nisha ameweka wazi kuwa hivi sasa yupo Kwenye Mahusiano na mwanaume wa maana ambaye amemzidi kiumri na wanasaidiana katika mambo mbali mbali.

Sina Bifu na Snura Ila Sio Rafiki Yangu- Nisha

Muigizaji wa Bongo movie Nisha aliyetoa nyimbo yake mpya ‘Bachela’ amefunguka kuhusu uhusiano wake na msanii wa Bongo fleva Snura na kusema hana bifu naye ila pia sio marafiki.

Ishu ya Snura na Nisha ilishika headlines sana wiki chache zilizopita baada ya Snura kuonekana ana uhusiano wa kimapenzi na Minu Calypto ambaye alikuwa ni mpenzi wa Nisha.

Taarifa zilienea na kudai kuwa Snura alimpindua NIsha kwa Minu ambaye alikuwa ni kiben 10 cha Nisha na hata maneno maneno yalisemwa Kwenye mitandao ya kijamii ingawa kila mmoja alisisitiza kuwa hana bifu na mwenzake.

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Millard Ayo Tv, Nisha ameweka wazi kuwa hana bifu na Snura wala hawana urafiki ila ni watu tu ambao wanafanya wote sanaa zao:

Mimi na Snura hatuna urafiki ni wasanii tu lakini pia hatuna Uhasama wowote wala bifu kwa sababu mwisho wa siku maisha yanaendelea kwa sababu aliyekuwa naye nilishaahana naye kabla hata hawajaanza mahusiano kwaiyo moyo wangu mweupe kwake”.

 

Amber Lulu: Nisha Alikuwa Anatembea na Young Dee Wakati Niko Naye

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Amber Lulu amepasua jipu na kumuanika hadharani msanii mwenzake Nisha na kudai alikuwa anaingilia penzi lake na staa wa Bongo fleva Young Dee kwa kumtongoza.

Amber Lulu aliyewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Young Dee amekiri kuwa wakati akiwa na Mahusiano na Young Dee alikuwa mtu wa michepuko sana kiasi ya kwamba alishawahi kubamba meseji za  Young Dee na Nisha wakichat kama wapenzi.

Amber Lulu alitoa siri hiyo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya EATV ambapo amesema ushahidi kuwa wawili hao walikuwa wakichepuka anao:

Nikiona meseji zao walikuwa wanavhat vizuri tu sema kiroho safi sikumaindi sana kwa sababu hatukuwa official na mimi mwenyewe nilikuwa na mambo yangu pembeni lakini nina ushahidi kuwa Nisha Kapita kwa Young Dee.

Nakusema ukweli Nisha fundi maana ana maneno matamu nini nilisoma mpaka mwenyewe nikakubali”.

Nisha alipoulizwa habari hiyo alikana kusema meseji alizoziona Amber Lulu zilikuwa ni meseji za kikazi tu lakini hajawahi kuwa na Mahusiano ya kimapenzi na Young Dee.

Sijawahi Kufunuliwa Sketi na Kiben-10: Snura

Msanii wa Bongo fleva Snura Mushi ametoa povu zito na kukana tuhuma za kutoka kimapenzi na msanii mwenzake wa Bongo fleva Minuh Calypto ambaye anajulikana kama kiben 10 kutokana na umri wake mdogo.

Wiki chache zilizopita Snurah alipata skendo hii nzito ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Minuh ambaye alikuwa anajulikana kama mpenzi wa muigizaji wa Bongo movie Nisha, ambapo stori zilianza kuenea mtandaoni kuwa Snurah kampindua Nisha na kumchukulia kiben-10 chake.

Ingawa Snurah alikataa tuhuma hizo na kudai ni habari za uongo kwani Minuh ni rafiki yake tu mambo yalichanganya zaidi pale ambapo picha zilisambaa kwenye mtandao zilizo muonyesha Minuh na Snurah wakiwa wanapeana mabusu mazito na wakiwa kwenye mahaba mazito lakini bado alizizdi kukataa mahusiano hayo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv kupitia kipindi cha FNL, Snura alitinga ndani ya studio hizo akiwa na Minuh Calypto huku wakiwa wamefika katika studio hizo kwa lengo moja tu nalo lilikuwa ni kukana tuhuma za mahusiano hayo ambapo alifunguka yafuatayo:

Kwanza msilazimishe vitu ambavyo havipo mahusiano yangu na Minu ni ya kawaida sana kama ambavyo nina weza kuwa nayo na mtu yoyote ambaye sina mahusiano naye ya kimapenzi yaani mahusiano ya kirafiki na ya kusaidiana na ya kishkaji ndo ninayo kwa Minu hayajavuka mpaka yaani hii nguo niiyovaa unaiona hii yaani hajawahi kuifunua”.

Minu alikubali kuwa aliwahi kuwa na mahusiano na Nisha lakini hana uhusiano wa kimapenzi na Snurah na lilisisitiza hajawhi kumfunua Snurah kwani anaogopa kupofuka macho kwa kumchungulia mdada mwenye umri mkubwa kupita yeye.

Nisha Amponda Bwana wa Snura Adai ni Kiben-10 Kula Kulala

Muigizaji  wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu mtandaoni Nisha Bebe amewatolea povu wanaume wote wanaopenda kulelewa na wamama watu wazima ambao wanajulikana kama viben-10 au Marioo au Serengeti boys.

Wiki chache zilizopita kuna stori ilitrend mtandaoni kuwa Nisha kaporwa kiben-10 chake na msanii wa Bongo fleva Snura Majanga. Kijana huyo anayejulikana kama Minu Calypto alikuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Nisha kwa mara ya kwanza ambaye alikuwa na umri mdogo kuliko yeye.

Minu hivi sasa kajiweka kwa mwanamke ambaye ni wazi kuwa ni mkubwa kuliko yeye maana Snura anaonekana kama mtu mzima kwa Minu. Baada ya picha za Minu na Snura kusambaa siku ya Valentine’s Day na kuthibitisha uhusiano wao, Nisha amewatolea povu zito viben-10

Kupitia kipindi cha FNL ya East Africa Tv, Nisha amemtolea povu aliyekuwa bwana ale Minu na kumuita kula kulala ambapo aliwaandikia:

Mnazingua kwaiyo mnadhani mimi naweza kutiwa stress na mwanaume kula kulala?nimeanza kusafiri tangu 2013 now ni 2018, Niacheni jamani tafadhali”.

Nisha amesema hawezi kukaa na kuumia kisa mwanaume ambaye alikuwa hamsaidii kitu chochote maishani mwake.

Nisha: Mnaosema Sina Shepu Nimepigwa Pasi Mnikome

Muigizaji wa Bongo movie Nisha amibuka tena na kumwaga povu zito kwa mashabiki zake baada ya kudai ameona maoni ya watu wengi wakimwambia kuwa kapigwa pasi yaani hana makalio.

Nisha alitoa povu hilo siku za nyuma kidogo ambapo ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa ambapo aliweka picha zake ambazo alikuwa amevaa gauni lake refu mpaka chini lililochora mwili wake ipasavyo ndipo kila mtu alipoanza kumsema hana mwili mzuri wa kuvalia gauni lile kwani amepigwa pasi.

Nisha alitokwa na povu zito baada ya kuona watu wanamsema na kudai hana shepu hivyo aliibuka na kusema shepu yake anaipenda ilivyo vile vile kwani sio feki kama shepu za wanawake wengi hapa mjini amabapo wengi wao hutumia madawa ya mchina kuongeza makalio:

Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe huu:

Halafu nyie mnaosema sina shepu sijui nimepigwa pasi mnikome, tukivaa vigodoro maneno mtu akivaa kama alivyo maneno, hemu chunguzeni wanawake wote wazuri duniani na wenye mashepu na status zao ndio wale wanaoishia kupiga picha za uchu, kujiuza, kuishi kwa kutegemea mabwana then angalia status za waliofanikiwa wote. Omba Mungu akupe afya njema, akili, imani, heshima, upendo, maarifa na kipato Sote tumeumbwa kwa mfano wake. Kutengeneza shepu ni dola 6000 tu lakini napenda Mungu alichonijalia na pia najivunia na nijajikubali”.

 

Nisha- Snura Hawezi Kuninyang’anya Bwana

Muigizaji wa Bongo movie Nisha amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na habari zinazozagaa mtandaoni kuwa msanii wa Bongo fleva na aliyekuwa rafiki yake Snura Mushi amemuibia bwana ake.

Habari za Nisha kunyakuliwa bwana na rafiki yake Snurah zilisambaa wiki iliyopita baada ya Snurah kuweka wazi uhusiano wake na kijana anayeitwa Minu Calypto ambaye mwanzoni alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nisha lakini baadae alionekana na Snurah.

Baada ya haari hizo kusambaa sana kwa kasi ya 4g Nisha mwenyewe ameamua kufunguka na kusema habari hizo hazina ukweli hata kidogo na kusisitiza kuwa hajachukuliwa bwana na mtu yeyote na hajawahi kugombea bwana na mtu.

Nisha amefunguka na kuiambia Enews ya East Africa TV kuwa habari hizo za yeye kuchukuliwa bwana na Snurah hazina ukweli wowote kwani yeye na mwanaume huyo waliachana miezi sita iliyopita na hata namba ya Simu ya Snurah yeye ndio aliyempatia.

Kwanza mimi sio mtu Wa kusimulia kila kitu ambacho ninacho huyo mkaka nilishaachana miezi sita sahivi Niko kwenye mahusiano mapya na mtu mwingine ambaye anajitambua, Snurah siwezi kumzungumzia sana kwasababu watu wanasema ameninichulia bwana na mimi nasema hajaninyang’anya bwana, kuninyang’anya ingekuwa kama bado Niko kwenye mahusiano na huyo mtu lakini tulishaachana”.

Lakini pia Nisha amesisitiza kuwa yeye na Snurah hawana bifu na pia bado ni marafiki wazuri tu bado wanaongea kwenye Simu kama kawaida na hata alivyomuomba namba ya yule mkaka hakuona soo kumpa kwa sababu walikuwa wameshaachana na yeye ameendelea na maisha mapya kwaiyo hakuna bifu kati yake na Snurah wala na Minu.

Snura Ajibu Atuhuma za Kuiba Mwanaume Wa Nisha

Msanii wa muziki bongo Snura Mushi maefunguka na kudai kuwa hana mahusiano yoyote na wanaume anaejulikana kwa jina la Minu kama ambavyo imekuwa ikisambaa katika mitandao kuwa anatemeba na mwanaume huyo kisa tu amemu-wish mwanaume huyo kheri katika siku yake ya kuzaliwa.snura amesema kuwa kati yake na minu kumekuwa na urafiki tu tena sio wa muda mrefu kama ambavyo watu wamekuwa wakizusha.

Mwanaume huyo ambae alikuwa mwanaume wa Nisha Bebe, msanii wa bongo movies inasemekana kwa aliibiwa na Snura kutoka kwa Nisha .

Tetesi hizo zilianza kusambaa baaada ya Snura kuweka picha ya kijana huyo na kuandika anampenda sana sana huku akimtakia kheri kwa siku yake ya kuzaliwa ndipo watu walipoanza ku-judge na kusema kuwa mwanaume huyo ameibwa kutoka kwa Nisha kwa sababu ni siku chache tu katika ukurasa wa Nisha aliandika akionekana kulalamika kuwa akuna watu wamemuibia mwanaume aliyekuwa nae.

Snura alisema kuwa minu na yeye walijuana baada ya nisha mwenyewe kumpa namba yake ili wafanye kazi ya muziki pamoja kwa sababu mwanaume huyo ni mwandishi wa mashairi.

huyo Minu sio mpenzi wangu na wala hatuna muda mrefu tangu nimejuana nae , kuna siku alinitafuta baada ya kupewa namba yangu na  nisha kwa sababu alipewa alikuwa ameandika wimbo ambao aliona mimi ninafaa kuuimba.sasa nimemtakaia kheri ya kuzaliwa na kumwambia kuwa ninampenda basi imekuwa kosa.

Nisha amekuwa akilalamika kila kukicha kuwa kila mwanaume anaekuwa nae katika mahusiano anachukuliwa na mwanamke mwenzie na kuacha mpweke.

 

 

Snurah Adaiwa Kunyakua ‘Kiben-10’ Cha Nisha

Muigizaji wa Bongo movie Nisha adaiwa kuwa katika kipindi kigumu kwa sasa baada ya kunyakuliwa mpenzi wake aliyekuwa na umri mdogo kuliko yeye kwa lugha ya mjini ‘kiben-10’ na msanii wa Bongo fleva Snurah Mushi.

Kuanzia wiki iliyopita habari za chino chino zilidai kuwa Snurah kamchukua bwana wa Nisha aliyekuwa naye kwa kipindi kirefu kidogo lakini inadaiwa kijana huyo ni kiben-10 ikimaanisha ana umri mdogo sana kwa wanawake hawa wawili.

Kijana huyo anayeitwa Minu anadaiwa kumwaga Nisha na kuhamisha majeshi yake kwa Snurah jambo ambalo linasemekana kuwa sio mara ya kwanza kutokea kwa Nisha kuibiwa kiben-10 chake kwani mwaka Jana alinyakuliwa tena Barakah the prince aliyekuwa mpenzi wake.

Minu ambaye kwa sasa ana uhusiano wa kimapenzi na Snurah Mushi amekuwa akitawala vichwa vya habari kwa skendo hii hasa kwa sababu hakuweza kujulikana kwa kupitia mziki wake pamoja na kuwa chino ya label ya mwanamuziki Christian Bella.

Pamoja na tuhuma hizo kumuelekea Snurah kama mwizi wa mwanaume wa Nisha, Snurah kupitia ukurasa wa Instagram alifunguka yafuatayo:

Moyo niache nimechoka mbona kuishi mwenyewe inatosha moyo uwapendao sio niache niache hujui kuchagua kule kule nilikoishia kumetosha sitaki Tena”.

 

“Sina Mimba mie” Nisha kaweka mambo wazi

Nisha hana mimba kamwe ndio ujumbe uliotufikia leo na kuweka mambo yote kwa wazi.

Akizungumza kwenye Millard Ayo, Staa huyo wa filamu anayejulikana kama Salma Jabu alieleza ya kwamba yeye hana mimba kamwe na picha aliyoieka kwenye mitandao ilikuwa yeye kwenye harakati za kikazi.

Kama balozi wa watoto wanao ishi katika mazingira ya ufukara, aliamua afanye uchunguzi ndio akuje kutoa filamu mpya na ndipo akabuni huyo character aliyeonekana kana kwamba alikuwa na mimba.

Mtazame kwenye hii video akiongelea jambo hilo kwa unenepa: