Vanessa Mdee awajibu mashabiki wanaodai kuwa Video yake mpya inafanana na Energy ya Keri Hilson

Mrembo Vanessa Mdee ameiwachia kazi yake mpya ‘Kisela’ ambayo imeonesha uwezo wa kufanya vyema ingawa wengi wanadai kuwa inafanana sana na ile ya Keri Hilson ‘Energy.’

Akiongea na kipindi cha The Playlist cha Times FM, Vanessa kwa mara ya kwanza alisema kuwa hakutarajia kuwa mashabiki wangefikiria kuwa aliiga wimbo huo wa Keri Hilson huku akiongeza kuwa uandishi wa script ya video ya wimbo wake ulifanywa na director wa video hiyo, Clarence Peter. Vmoney alisema,

“To be honest mimi napenda sana huo wimbo, I love the video, I love Keri Hilson but I did,’t think about that video at all. In fact hii script mimi sikuandika kabisa, usually na play part kwenye script write lakini sikuandika kabisa, aliandika Clarence, alinitumia the hall script. When I was doing I said okay great but now when people started to refer nikasema duuh! Maybe but there’s no original concept,”

 

Hata hivyo kunauwezekano kuwa inspiration ilitoka kwenye wimbo huo wa Energy kwani pia maudhui yake yanaambatana.