Ni kweli kuwa Vanessa Mdee na Juma Jux sababu ya Jacqueline Patrick?

Kuna fununu kuwa Vanessa Mdee na Juma Jux waliachana kutokana na sababu zisijojulikana! Hata hivyo kulingana na Ubuyu wa global publishers, kunauwezekano kuwa wawili hawa waliachana kwa sababu ya aliyekuwa mpenzi wa Juma Jux wa zamani, Jacqueline Patrick ‘Jack’.

Juma Jux na aliyekuwa mpenzi wake, Jacqueline Patrick ‘Jack’.

Jacqueline Patrick ambaye anatarajiwa kuachiliwa kutoka sasa za gereza nchini China, amesemekana kuwa yeye ndiye chanzo cha wawili hawa kuachana. Kulingana na habari mitandaoni, jack anatarajiwa kuachiliwa mwezi huu na ndio maana Jux yuko China akimgonja mrembo aliyetiwa ndani baada ya kupatwa akisafirisha madawa ya kulevya China.

Chanzo cha maneno haya kiliwambia Global publishers Kuwa;

“Unajua Jack anatarajiwa kutoka gerezani ndani ya mwezi huu na ikumbukwe wakati anafungwa alikuwa bado kwenye uhusiano wa kimapenzi na Jux hivyo ndiyo maana mapenzi ya Jux na Vanessa yamekwisha. Kwa sasa Jux yupo nchini China na inasemekana atarudi na Jack kwani inadaiwa ameenda huko kwa ajili ya shughuli zake binafsi lakini pia anamsubiria Jack atoke lupango na wataendelea na mapenzi yao kama zamani,”

Hata hivyo Juma Jux alikataa kudhibitisha ikiwa habari hizi ni za kweli.

“Vanessa Mdee ananipa stress” Lulu Diva afunguka

Mwanamziki Lulu Diva ambaye anaonekana kutamba Afrika Mashariki kupitia wimbo wake Wa utamu amedai kuwa Vanessa Mdee ni mwanamke anayempa stress kila kukicha.

Vanessa Mdee

Mrembo huyu alisema haya katika mahojiano yake na Uwazi Showbiz. Kulingana na Lulu Diva, Vanessa Mdee ndiye ni mwanamziki ambaye ameweza kupenya kwenye muziki haraka huku akipata kollabo na wasanii wa kutoka inje – kitu ambacho wasanii wa kike bado hawajaweza kufanya. Lulu alisema:

“Bongo kwa wanamuziki wa kike kiukweli anayenipa stress ni Vee, kila mtu anafahamu kuwa ni mkali na anajituma kwenye muziki wake, sasa mimi malengo yangu ni kufanya kazi kwa juhudi ili kufika mbali, kwanza kuwa hapo alipo yeye na baadaye kupita zaidi,“

Hata hivyo Lulu Diva alisema kuwa anandoto za
kufanya muziki wa kimataifa siku moja.

Vanessa Mdee awajibu mashabiki wanaodai kuwa Video yake mpya inafanana na Energy ya Keri Hilson

Mrembo Vanessa Mdee ameiwachia kazi yake mpya ‘Kisela’ ambayo imeonesha uwezo wa kufanya vyema ingawa wengi wanadai kuwa inafanana sana na ile ya Keri Hilson ‘Energy.’

Akiongea na kipindi cha The Playlist cha Times FM, Vanessa kwa mara ya kwanza alisema kuwa hakutarajia kuwa mashabiki wangefikiria kuwa aliiga wimbo huo wa Keri Hilson huku akiongeza kuwa uandishi wa script ya video ya wimbo wake ulifanywa na director wa video hiyo, Clarence Peter. Vmoney alisema,

“To be honest mimi napenda sana huo wimbo, I love the video, I love Keri Hilson but I did,’t think about that video at all. In fact hii script mimi sikuandika kabisa, usually na play part kwenye script write lakini sikuandika kabisa, aliandika Clarence, alinitumia the hall script. When I was doing I said okay great but now when people started to refer nikasema duuh! Maybe but there’s no original concept,”

 

Hata hivyo kunauwezekano kuwa inspiration ilitoka kwenye wimbo huo wa Energy kwani pia maudhui yake yanaambatana.