Wellu Sengo Amkingia Kifua Steve Nyerere

Muigizaji wa Bongo movie Wellu Sengo ameibuka na kumkingia kifua Baba Watoto Wake Steve Nyerere kwa kusema haoni tatizo kwa mambo yake anayoyafanya mitandaoni hasa kuropoka juu ya ishu za mastaa wenzake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Wellu alisema kuwa hawezi kupitia kila anachokifanya Steve mitandaoni ila kama kuna kitu anaona kina tatizo, huwa anamshauri.

Sioni sababu na siwezi kupitia kila kitu anachokifanya Steve mtandaoni. Unajua kila mtu ana hulka yake, labda na yeye ndivyo alivyo. Kwa hiyo mimi huwa naangalia vitu muhimu kama anakosea ndiyo tunakaa, tunashauriana“.

Stwvw Nyerere amekuwa akipingwa sana na mashabiki wengi wa Mitandao kutokana na misimamo yake ya kisiasa Lakini pia Hivi karibuni alipatwa na Skendo ya mwaka Baada ya kutoa kauli kuhusu Ommy Dimpoz kuwa hatoweza kuimba tena.

Maneno ya Mitandao Yamficha Mtoto wa Wellu Sengo.

Mwanadada kutoka bongo movies Wellu Sengo amefunguka na kusema kuwa kwa muda wa mwaka mmoja alimuweka mtoto wake chini ya kapeti na kumficha ili tu kuogopa maneno ya waja yanayozungumzwa katika mitandao ya kijamii.

Mtoto huyo wa Wellu ambae alibahatika kuzaa na msanii mwenzie steve nyerere alikuja kujuliakna kwa watu na katika mitandao baada ya kutimiza mwaka mmoja na ndipo watu wengi walipokuja kujua pia pia kuwa ni mtoto wa steve nyerere .

sikumuonyesha mwanangu katika mitandao ya kijamii kwa sababu ya kuogopa maneno ya waja,lakini pia napedna kuwa kimya ili watu waone matokeo.Lakini pia kuhusu ndoa siwezi kuzungumza chochote.