Msanii Whozu Akiri Kumzimia Mimi Mars

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Whozu ambaye alijizolea umaarufu baada ya kuachia wimbo wa ‘This is Tanzania’ amefunguka na kuweka wazi kuwa anamzimia vibaya mbo Msanii mwenzake Mimi Mars.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Whozu anayefanya vyema na kibao chake cha ‘Huendi Mbinguni’ amesema amesha mfungukia Mimi Mars juu ya mapenzi yake kwake:

Mimi Mars mwenyewe nimeshangazwa mwambia kuwa nampenda na nimesha mtumia meseji nyingi kuwa nampenda lakini mwisho wa siku akaniambia atanifikiria kwaiyo mpaka leo nasikilizia bado ananifikiria labda huwezi jua siku yoyote Mzee naweza kukaa pale”.

Lakini pia Whozu alitoa ushauri kwa wanaume wengine kutoogopa wanawake na kuacha kuwafuata kuwaambia ya moyoni kwa sababu labda Wazuri sana kwani inaweza ikawa  Bahati yako siku hiyo ukakubaliwa.