Mimi Mars Akiri Kuwa Ameshawahi Kuwa Mmbea Sana

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Marianne Mdee maarufu kama Mimi Mars amefunguka na kuweka wazi kuwa alivyokuwa Mtoto alikuwa na tabia za umbea.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Mimi Mars ambaye kwa sasa ana­tamba na kibao chake cha Kodoo alisema zamani alikuwa na tabia ya kuongeaongea hovyo kiasi cha kuwakera wen­gi lakini anashukuru Mungu alivyokua hiyo tabia akaachana nayo.

Kweli ukiwa na utoto unakuwa na mambo mengi lakini ukikua unaacha, tabia yangu ya uropokaji na um­beya vilinifanya niogopwe. Yaani nikiwa nimekaa sehemu watu wananik­wepa lakini najua ilikuwa utoto tu, sasa nimekuwa nimeacha“.

Mimi Mars ameongeza kuwa tabia hiyo ya umbea ilikuwa inamkera sana Dada yake staa wa Bongo fleva Vanessa Mdee kiasi ya kwamba walikuwa wanamtenga walipokuwa wanataka kuzungumza Mambo yao.

Mimi Mars Afungukia Furaha Aliyonayo Kutokana na Kuwa Single

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Marianne Mdee maarufu kama Mimi Mars amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna kitu kinachompa furaha kama kuwa single kwa sababu yupo huru kufanya kazi zake vizuri.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Showbiz, Mimi Mars alisema, aliamua kuishi peke yake bila mwanaume kwa sababu ameshawahi kuumizwa na aliokuwa akiwapenda hivyo kumfanya kuwa mpweke na kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

Niliishia kuambulia maumivu tu kutokana na kuwa na wanaume wasiokuwa waaminifu, nikaona hapana, kwa nini niendelee kuteseka wakati kuna maisha baada ya mapenzi? Hivyo nimeamua kuishi mwenyewe mpaka pale nitakapompata mtu sahihi, nayafurahia haya maisha kwa sasa”.

Mimi Mars ameshawahi kutajwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Staa wa muziki wa hip hop nchini Kutokea katika Kundi la Weusi Joh Makini.

 

 

Mimi Mars Amkana Rammy Gallis Kweupe

Siku chache baada ya msanii wa bongo movies Rammy Gallis kufunguka na kusema kuwa moja ya wasanii wa kike anaowakubali sana katika game la bongo fleva ni Mimi mars na kusema kuwa anatamani sana kuonana nae siku moja na hata kutaka kuwa mpenzi wake.

mimi mars nae alifunguka na kusema kuwa kwa upande wake hawezi kukubali kiurahisi kiasi icho kwa sababau hamjui Rammy gallis zaidi ya kumsikia sana kipindi ambacho kulikuwa na msiba wa mmwanadada Agness masogange na hiyo ni kutokana na skendo yake ya kuanguka kwa kuzimia ndipo alipomfahamu Rammy.

jaman hapana yule kaka sijawahi kusemakokote na kwanza nilimuoa kwa mara ya kwanza katika msiba wa agness alipokuwa amezimia huku akiwa ameshika kitambaa,  na wala sio vinginevyo kabisa, sijawahi kumtajasehemu yoyote ile , sijawahi kusema ninampenda au ninataka kuonana nae.

Katika moja ya mahojiano ya rammy hapa karibuni alisema kuwa yeye anampenda mimi marsa kwa sababu hata yeye aliwahi kumsikia dada huyo akisema anampenda.

Sioni Tatizo Kurudia Nguo- Mimi Mars

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Marianne Mdee maarufu kama Mimi Mars ameibuka na kuweka wazi kuwa haoni tatizo kwake binafsi kurudia nguo hata kama yeye ni staa kwani ni jambo la kawaida.

Mimi Mars ameongea hayo baada ya mashabiki kumtolea povu zito baada ya kuonekana anerudia nguo alipokuwa kwenye mahojiano na runinga moja nchini.

Global Publishers wanaripoti kuwa Mimi Mars alionekana akiwa amevaa gauni pamoja na nywele hizohizo mwezi wa kwanza mwaka huu, alipokuwa kwenye uzinduzi wa albamu ya dada yake iliyojulikana kwa jina la Money Mondays na juzikati akarudia tena kwenye mahojiano hali iliyosababisha watu kumshambulia kwamba inakuwaje anarudia mavazi wakati yeye ni staa.

Binafsi sioni tatizo kurudia nguo ila watu wanaongea kwa sababu mimi ni staa, niwaombe tu mashabiki zangu tufuatiliane kwenye kazi na siyo mambo yasiyokuwa na maana”.

Wasanii wengi wamekuwa wakikosolewa kwa tabia ya kurudia nguo ambapo mashabiki wengi wamewataka Mastaa kuwa smart na kupiga pamba na kuwa na muonekana wa kistaa.

 

Mimi Mars-Napenda Sana Mapenzi

Mwanamuziki wa Bongo fleva na Mshehereshaji (MC) maarufu kama Mimi Mars amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna kitu anapenda duniani kama Mapenzi.

Mimi Mars amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, ambapo amekiri kuwa yeye ni mtu wa mapenzi sana kiasi ya kwamba hata akikutana na jambo lolote linalohusu mapenzi basi huwa Makini.

Mimi napenda sana mapenzi hata kama kuna story ya mapenzi kuna sehemu imeisha ukianza kuwa na Mahusiano na mtu mwingine unaanza upyaa, ina maana uneshasahau yale ya nyuma kimeanza upya Coz you know mapenzi yanarun dunia”.

Mimi Mars anayetokea Kwenye Familia ya Kimuziki kuanzia dada yake Vanessa Mdee anayefanya muziki wa Bongo fleva mpaka dada yake mwingine ambaye pia ni msanii wa nyimbo za injili, ameendelea kufanya vyema na ngoma yake ya ‘Kodo’.

 

Vanessa Mdee Amaliza Bifu Lake na Mimi Mars

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money amefunguka na kuweka wazi kuwa ameamua kumaliza bifu lililokuwepo kati yake na mdogo wake ambaye pia ni msanii mwenzake Mimi Mars.

Vanessa Mdee ameweka wazi kuwa yeye pamoja na ndugu yake huyo kama ilivyokuwa katika familia yoyote kulikuwa na migongano lakini amefikia uamuzi wa kumaliza bifu hilo na kwa sasa wako vizuri.

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Vanessa Mdee Vanessa amesema kuwa ameamua kumaliza tofauti kati yake na ndugu yake huyo kwa kuwa wao ni ndugu hivyo hakuna maana yoyote wao kutofautiana.

Naona ni jambo jema kwa kuwa mimi na mdogo wangu tulikuwa hatupo pamoja kutokana na sababu tu ambazo hazina msingi. Kwa hiyo nimeona tumalize bifu letu na tuendelee kupeana sapoti katika kazi zetu japokuwa kila mmoja anafanya muziki wake“.

 

Msanii Whozu Akiri Kumzimia Mimi Mars

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Whozu ambaye alijizolea umaarufu baada ya kuachia wimbo wa ‘This is Tanzania’ amefunguka na kuweka wazi kuwa anamzimia vibaya mbo Msanii mwenzake Mimi Mars.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Whozu anayefanya vyema na kibao chake cha ‘Huendi Mbinguni’ amesema amesha mfungukia Mimi Mars juu ya mapenzi yake kwake:

Mimi Mars mwenyewe nimeshangazwa mwambia kuwa nampenda na nimesha mtumia meseji nyingi kuwa nampenda lakini mwisho wa siku akaniambia atanifikiria kwaiyo mpaka leo nasikilizia bado ananifikiria labda huwezi jua siku yoyote Mzee naweza kukaa pale”.

Lakini pia Whozu alitoa ushauri kwa wanaume wengine kutoogopa wanawake na kuacha kuwafuata kuwaambia ya moyoni kwa sababu labda Wazuri sana kwani inaweza ikawa  Bahati yako siku hiyo ukakubaliwa.

Ukinileta Huyo Mtu Sasa hivi Nitafunga Ndoa:-mimi mars

Mwana dada Mimi Mars amefanya mahjiano na moja ya waandishi wa habari na kusema kuwa pamoja na kwamba kumekuwa na wimbi la wasanii wengi kwa sasa wanafunga ndoa lakini kwake yeye anaona bado muda kwa sababu anasubiri mtu mwenyewe wa kufung nae ndoa ajitokeze na ndio awaze kufunga ndoa.

Mimi Mars amabe alishawahi kusikika akisema kuwa mapenzi yamekuwa yakimuumiza sana anasema kuwa bado kwa sasa hajapata mtu wa kumuoa hataki kuwa na papara kwa sababu mapenzi yalishamuumiza.

Alipoulizwa mimi mars kuhusu lini na yeye atafunga ndoa kama ilivyo sasa kwa wasanii wengi kufunga ndoa aliwajibu hivi:-

bado kidogo kwanza tumsubitie huyo mtu afike na kisha ndo tuanze kujua tunafunga ndoa lini,kidogo si siku yoyote lakini kama utaniletea huyo mtu sasa hivi haina shida basi mapema.

Wasanii wengi wa bongo sasa hivi wameanza kujiingiza katika mjaukumu ya kifamilia kwa kufanikisha swala la zima la kuingia katika mhusiano na kufunga ndoa.

 

Mimi Mars- Napenda Kufanya Kazi Na Wasanii Wengine

Mwanamuziki wa Bongo fleva Marianne Mdee maarufu kama Mimi Mars amefunguka na kuweka wazi kuwa moja kati ya vitu anavyopenda ni kishirikiana na wasanii wenzake kumaanisha kufanya kolabo.

Mimi mars ameweka wazi kuwa kufanya Kolabo na wasanii mbali mbali ku amefanya ajisikie vizuri kwani anaamini kuwa ushirikiano kati ya wasanii ni kitu kizuri sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Mikito Nusu nusu Mimi Mars ambaye hivi karibuni amepiga kolabo na Frankie Maston na Yeyo Leslie, wa ngoma iitwayo Mi Nawe, amesema kushirikiana kwenye muziki ni kitu kizuri na ikitokea akihitajika na mtu.

Mimi Mars alijizoelea umaarufu baada ya kutoa Single yake ya kwanza lakini moja ya kitu ambacho kilimpa umaarufu zaidi ni kuwa dada wa staa wa Bongo fleva Vanessa Mdee.

Mimi Mars Kurejea Kwenye Utangazaji Tena

Mwanadada mimi mars amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi karibuni atarudi kwenye tasnia ya utangazaji aliokuwa kiufanya hapo mwanzo kipindi hajajikita sana katika muziki.mimi mars amae hapo mwanzo alikuwa akitangazaji kipindi cha weekend gossip kupitia tv 1 anasema kuwa anatarajia kurudi tena katika fani yake hiyo.

Mipango ya kurudi huko bado hipo na chamsningi ni ku-keep up na mimi tu ili kujua ni lini na wapi kitaanza na sehemu gani.

Hakutakuwa na utofauti sana kwa sababu kupitia kile kiindi ndipo watu wemgi walikuwa wakinijua mimi mars  na mashabiki wangu wengi niliwapta kupitia hapo, mapka ninaingia katika muziki.–Alifunguka MImi Mars alipokuwa akiongea na Bongo5.

Mimi Mars: Sitaki Kuolewa na Mwanaume Mpare

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Papara’ Mimi Mars ambaye pia ni mdogo wa staa wa Bongo fleva Vanessa Mdee, amefunguka na kuweka wazi kuwa hataki Kuolewa na mwanaume kabila la Wapare.

Mimi Mars amesema kuwa hategemei na wala hataki kuolewa na mwanaume kutoka katika kabila la wapare kwa sababu yeye mwenyewe ni mpare na kuna baadhi ya tabia za wapare anazijua na hazimpendezi.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Mimi Mars pia ametaja Makabila mengine kama wachaga ambayo nayo amekiri hatorudia Tena kuwa nao:

Kwa sababu mimi mwenyewe ni mpare kwaiyo tabia za wanaume wa kipare kidooogo nazijua alafu wanasemega ile mafahari wawili hawawezi kukaa kwenye zizi moja kwaiyo najua tutashindwana tu maana wote ni wabishi, wabahili kwaiyo tutashindwana tu na sio kwa ubaya ila mimi tu sipendi.

Lakini pia Mimi Mars ameweka wazi kuwa kwa sasa hana mpenzi yupo single:

Hapana mimi sahivi sina mtu niko peke yangu sina mchumba”.

 

Mimi Mars: Sina Papara Na Mapenzi

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri kwa hivi sasa na ngoma yake mpya ya papara Mimi Mars amekiri kuwa hana haraka ya kihivyo ya kuwa kwenye Mahusiano ya kimapenzi.

Mimi Mars aliyejipatia umaarufu na ngoma yake ya kwanza ya shupa Lakini pia ni mdogo wa staa wa Bongo fleva Vanessa Mdee, amekiri kuwa ana pressure kubwa ya kuwa kwenye mahusiano na kuyaweka public kutoka katika mashabiki zake.

Siku za hivi karibuni Mimi Mars alikumbwa na skendo ya kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na Diamond Platnumz na hata rapa Joh Makini na hata shemeji yake Jux Tetesi za Mahusiano ambazo alizikana.

Kwenye Interview aliyofanya na Bongo 5 Mimi Mars amefunguka pia hata kama akiwa Kwenye Mahusiano hatapenda kuweka kila kitu public bali atataka Mahusiano Yake yawe private:

Hapana kwa sasa siko kwenye mahusiano lakini naona hata kama nikiingia Kwenye Mahusiano itakuwa ngumu kwangu mimi kuyaanika kwa sababu naona tayari maisha yangu yote yako public kwaiyo nitataka hata nikirudi nyumbani niwe na angalau kitu changu peke yangu ambacho mimi mwenyewe nakijua na pia inanisaidia maana ni kuweka mahusiano wazi inanisaidia kidogo maana Mahusiano hakuwa wazi inaleta matatizo kidogo”.

 

 

Mimi Mars Afunguka Tetesi za Vee Kuwa Mjamzito.

Msanii wa muziki  bongo fleva mimi mars amefunguka na kumtetea dadake vannesa mdee kutokana na tetesi zilizokuwa zimezuka siku za nyuma kidogo kuhusu Vannesa kuonekana kuwa ni mjamzito,Mimi Mars amesema kuwa dada ake amekuwa akila sana kwa sasa hivi na ndio maana amekuwa akiongezeka kila siku lakini sio kwamba vee ana mimba.

Akiongea na Funiko base ya Radio Five, Mimi Mars anasema kuwa kupenda kula kwa Vannesa kunasababisha watu kuhisi kuwa dada ake ni mjamzito lakini sio kweli na ni kitu ambacho hakiwezekani.

Hapana haiwezi kutokea,namuoa kila siku ni kwamba  anakula sana, mahaba ni mengi sana kwaio wanafurahia sana lakini sio hivyo na wala hana mimba .-Alifunguka Mimi Mars.

Vannesa ambae yuko katika mahusiano na msanii mwenzake Jux wamekuwa katika mapenzi kwa muda mrefu ambapo siku za nyumba ilitokea picha iliyomuonyesha Vannesa sehemu yake ya tumbo kuwa kubwa  na kusababisha watu kuhisi kuwa ni mjamzito.

Mimi Mars na Vannesa ni ndugu wa familia moja na wamekuwa karibu katika kusaidia kimuziki ingawa hawajawahi kufanya kazi ya muziki kwa pamoja.

Mimi Mars Amefungukia Mahusiano Yake na Diamond

Mwanamuziki wa Bongo fleva Mimi Mars aliye chini ya Mdee Music anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘papara’ amefunguka na kueleza uhusiano alionao na supastaa wa mziki wa Bongo fleva, Diamond Platnumz.

Kumekuwa na taarifa nyingi ambazo zimedai kuwa Mimi Mars ametoka kimapenzi na msanii Diamond Platnumz.

Mimi Mars amekataa kata kata habari hiyo na kuiita ya uongo kwani anajua kwa nini watu walizusha jambo hilo ambapo amedai kuwa kuna video ilisambaa mtandaoni akicheza wimbo wa Diamond baada ya kuona vile wao wakazua yao.

Kwenye Interview aliyofanya na Times Fm kupitia kipindi chao cha The Playlist Mimi mars amefunguka haya zaidi juu ya tuhuma hizo:

Taarifa hizo hazina ukweli kabisa kwanza cha kushangaza wakati nacheza huo wimbo hata sikujua kuwa ni Diamond, nilikuwa nimeenda kwa fundi akawa ameweka mziki akasema hebu cheza kidogo so I was just dancing kwaiyo hakuna ishu yoyote mbaya”.

Mimi Mars ambaye ni mdogo wa msanii Vanessa Mdee anafanya vizuri kwenye gemu na sio kuimba tu lakini pia Mimi ana kipaji cha utangazaji Mc kitu ambacho watu wengi hawakijui.

Siwezi Kukaa Sehemu na Jux Kama Vannesa Hayupo.

Mimi mars ambae ni mdogo  wake na Vannesa amefunguka na kusema kuwa hawezi hata siku moja kukaa sehemu na shemeji yake Jux ikiwa dada  hayupo katika eneo hilo.Mimi Mars amesema kuwa hata kipindi dada yake alipokuwa hayuko sawa kimahusiano na Jux ilikuwa ni vigumu sana kwa wawili hao kuwa pamoja labda kama watakutana tu studio na maeneo ya kazi.

Mimi na Jux hatuna ukaribu labda tumekutana tu studio au sehemu ya kazi lakini tofauti na hapo siwezi kukaa sehemu na Jux alafu Vannesa hayupo, na hata studio tukikutana ni kusaidia kazi  na kupeana tu ile hi basi ,ila  hicho ni kitu ambacho hatakaa haweze.

Mimi Mars amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana mahusiano kabisa ingawa amekuwa akikutana na tetesi nyingi sana za yeye kutoka kimapenzi na wasanii wenzake lakin habari hizo zote hazina ukweli wowote na kamwe hawezi kutoka kimapenzi na mtu maarufu kwa sababu anaamini hakuna kazi itakayofanyika.

Kipindi cha nyuma kidogo mimi mars alishawahi kusingiziwa kutoka kimapenzi na Diamond Platinumz,Quicker Racka na hata Joh Makini lakini  mimi

Sina Muda wa Mapenzi Kwa Sasa:Mimi Mars

Msanii  mrembo kutoka familia ya Mdee Music Mimi Mars amefunguka hali yake ya mahusiano kwa sasa na kusema kuwa kwa sasa hana muda wa kuendekeza mapenzi zaidi ya kufanya kazi kwa sababu bado kuna vigeoz anataka kwa mwanaume ingawa anapoaamua kuvitaja hadharani wengi wanamfata na kumwambia kuwa hata wao pia wanavyo.

Akiongea katika station moja ya radio iliyopo mtandaoni Mimi Mars alisema kuwa huwa hatumiI muda wake mwingi katika kujihusisha na mapenzi zaidi ya kazi na hata siku ya wapendanao alilala siku nzima na kisha kwenda studio.

Valentine yangu nililala tu siku nzima na baada ya hapo nilamka na kwenda studio kumalizaia mabo fluani kuhusu papara,kwangu hiyo ni siku ya kawaida tu kwa sababu sisis watu tusiokuwa na mahusiano ni kawaida tu.

Baada ta sitamani kumekuwa na Dm’s nyingi sana wakitaka kuingia katika mahusiano na mimi hivyo nikaamua kuja na hiyo papara kwa sababu nataka kuwaionyesha kwamba jamani eeh mimi sina mapapara na mabo ya mapenzi na sina muda na mambo hayo kwa sasa zaidi ya ku-chill tu.

sitaki kuwa katika situationyoyote ya mapenzi kwa sasa hiyo njia imefungwa labda baadae kidogo kama katikati ta mwaka hivi.

Akiongezea kwa kutaja sifa za mwanaume anayempenda Mimi Mars alisema kuwa anapenda mwanaume ambae:

hasiwe mtu maarufu lakini pia awe tu ni mtu anaejielewa sana na awe na goals zake na awe anafight kuzi-make happen lakini pia awe na hofu ya mungu ,na kwenye sura kidogo awe amaizing.