Wasafi Festival Kuwashusha Wizkid na Mr. Eazi

Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa staa wa muziki kutoka Nigeria  Wizkid kwa ajili ya kuperfom katika tamasha la Wasafi Festival.

Diamond Platnumz  amethibitisha hilo kupitia ukurasa wa Instagram baada ya ku-comment kwenye post ya Rayvanny ambayo alipost video fupi ikiwaoyesha Diamond na Wizkid muda mfupi baada ya kumalizika kwa tamasha kubwa la muziki la One African Music Festival lililofanyika Dubai wikiendi iliyopita.

Kwenye video hiyo Diamond alithibitisha kuwa atamshusha msanii huyo mkubwa Afrika kwenye tamasha hilo litakalofanyika Dar Es Salaam baada ya kuzunguka mikoa mingine.

Lakini pia na msanii Harmonize ameamua kuweka wazi meseji zake alizokuwa anawasiliana na msanii kutoka Nigeria akiomba kuja kushiriki angalau katika moja ya tamasha la Wasafi Festival Tanzania.

Dayna Nyange Asafisha Nyota na Wizkid Nigeria

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva ambaye ni hitmaker wa Mafungu ya nyanya, Dayna Nyange amefunguka na kueleza jinsi alivyokutana na staa wa nchini Nigeria Wizkid.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Dayna amefunguka jinsi alivyokutana na Wizkid ambaye  alimpokea vizuri na hata sapoti kubwa aliipata kutoka kwa Wizkid.

Siwezi kusema kuwa nipo njiani kutoa naye wimbo, hiyo inabaki kimenejimenti kwa sasa lakini ninachotaka kushea na nyinyi, jamaa (Wizkid) ameweka heshima ya aina yake kwao, amekuwa ni mtu wa watu na hata nilivyokutana naye kila mmoja alikuwa akijiuliza huyu nani ametoka wapi, kumbe ni Mbongo mimi, haaa haaa.

Mbali na kukutana naye na kuzungumza naye mawili matatu, nilibahatika kutembelea redio zao, yaani karibu kila redio ni kama wameweka kautamaduni kao, kuna picha kubwa za wasanii wao wanaoiwakilisha nchi, kuna P Square, Wizkid, Davido, Yemi na wengine wengi tofauti na hapa Bongo kikubwa utakutana na saini za wanamuziki tu”.

Dayna ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu ameachia ngoma yake mpya ya ‘Salama’ ambayo mpaka sasa inaendelea kufanya vizuri.