Amber Lulu Adai Kuwa Akimwagwa na Prezzo Atarudi Kwa Young Dee

Muuza nyago kwenye video au video queen maarufu aliyegeukia Bongo fleva, Amber Lulu amefunguka na kudai kuwa endapo Prezzo atamwaga basi hataona hiyana kurudi kwa Young Dee.

Amber Lulu amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Prezzo msanii maarufu kutoka Kenya kwa miezi kadhaa sasa lakini imekuwa ikionekana kuwa mpenzi wake wa zamani rapa Young Dee anahusishwa sana au anatajwa sana kwenye mahusiano hayo.

Amber Lulu na Young Dee walikuwa wapenzi kwa kipindi kirefu ambapo kutoka katika vyanzo mbali mbali vilidai kuwa Amber alimpenda sana Young Dee ingawa alikuwa anamfanyia ndivyo sivyo, kuna siku hadi rafiki wa karibu wa Amber Lulu, Gigy Money alisikiaka akisema “Amber Lulu anampenda sana Young Dee sema tu Young D mwenyewe hataki kitulia”.

Hata hivyo hapa kati Young D na Amber Lulu waliingia katika majibizano ya kwenye mitandao ya kijamii baada ya kurushiana maneno mazito ambapo kisa kilianza baada ya  Amber Lulu kumtolea povu mtu alipomlinganisha Prezzo na Young Dee na kudai asimlinganishe mpenzi wake Prezzo na vitu vya ajabu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Amber Lulu alimtolea povu shabiki wake ambaye alimhoji endapo kuwa tetesi zinazoenea mtandaoni kuwa ameachana na mpenzi wake Prezzo zina ukweli wowote, badala ya Amber luli kumjibu shabiki huyo kama jibu ni ndiyo au hapana badala yake alimtolea povu zito na kuandika “Ndiyo siku nikiachana na Prezzo lazima nitarudiana na Young Dee”.

 

Young D Kanizidi Tattoo Na Umri Lakini Kuchana Haniwezi- Young Killer

Msanii wa bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap, Young Killer Msodoki amefunguka na kudai kuwa msanii mwenzake Young D hajamzidi kitu zaidi ya tattoo za mwilini lakini kwenye kurap na kuchana hawezi kumfikia hata siku moja.

Siku za hivi karibuni wasanii hawa wawili wamekuwa kwenye bifu zito sana la kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii huku kila mmoja wao akidai ana uwezo mkubwa wa kuimba na kuchana kuliko mwenzake.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Dizzim Tv, Young Killer alifunguka yafuatayo kuhusiana na bifu lake na Young D ambalo lilipelekea Young D kumtukana matusi ya nguo keen he kipindi cha Friday Night Live:

Unajua huu utamaduni wetu wa hip hop unaruhusiwa kumuweka mtu sawa kama hayupo sawa ili mradi haumtukani na vitu kama hivyo lakini mimi Young D alikuwa amenitukana matusi ya ndani kabisa, basi pale pale studio nikamuuliza akisema hataki kufananishwa na mimi anakuwa anamaanisha kwenye sekta gani labda? Lakini sikupata jibu ikabidi niseme tu ilimradi tupo studio DJ atuwekee biti tuchane, tumewekewa biti mi nimechana mwenzangu anaambiwa achane kuvhana hawezi basi hapo ndo wenyewe muone kuwa hatufai kufananishwa yaani unajiita rapa lakini kuchana huwezi basi mimi naona yeye alichonizidi ni tattoo mwilini na umri wake umeenda kidogo kuliko mimi lakini kuchana hawezi kunifikia hata siku moja nimeshamdhihirishia hilo”.

Young Killer ameongelea pia wimbo wake mpya alioshirikishwa na Diamond lakini pia aliongelea mchango mkubwa wa Fid q katika mziki wake na mafanikio yake kisanaa.