Young Tusso Bado Anazimika na Penzi la Wolper

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayejulikana kama Young Tusso ambaye alijipatia umaarufu miaka ya nyuma kwa mara ya kwanza baada ya kutoa wimbo wake aliouita Jacqueline Wolper.

Young Tusso aliupa wimbo huo jina la Wolper kwa sababu wimbo mzima alimuimba Wolper na kufunguka jinsi gani anamkubali na yuko tayari hata kumuoa siku moja endapo atapata nafasi kwake.

Young Tusso Akiwa na Wolper

Baada ya kusikia wimbo huo na kuvuma sana Wolper alikiri kuvutiwa na wimbo na alisema anamkubali Young Tusso kama shabiki wake lakini pia alisisitiza kuwa na yeye pia ni shabiki wa kazi za Young Tusso.

Lakini tangu hapo Young Tusso hakukomea kumtaja Wolper kwenye nyimbo zake nyingine ameendelea kumtaja Wolper Kwenye nyimbo zake nyingine kama ishara ya kwamba anampenda kimapenzi jambo ambalo baadhi ya wadau wa muziki wamedai inamuharibia biashara.

Kitu ambacho Young Tusso amekataa kata kata kwani amedai anaongea kuhusu mambo mengine mengi zaidi ya kumuongelea Wolper hivyo itakuwa ngumu kwa kufeli kimuziki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Young Tusso alifunguka yafuatayo:

Kwanza ukisikiliza wimbo wangu wa ‘Kaza roho’ ni wimbo ambao nimezungumza vitu vingi sana sijui kwa nini watu wameishika sehemu niliyomtaja Wolper  Alafu isitoshe sioni tatizo kumtaja kwani sijamtaja kwa ubaya ni feelings tu ninaepress mapenzi yangu kwake”.