Tangu Nikiwa Mtoto Nilikuwa Naongelewa, Mama Aliniambi kwa sababu Nina Kitu Special:-Hamisa

Mwanadada Hamisa Mobeto jana laipokuwa katika kampeni ya SMART na wasanii mbalimbali alipata bahati ya kuulizwa swali na waandishi wa habari  kuhusu yeye kuwa akiongelewa katika mitandao ya kijamii na ndipo aliposema kuwa kwake ni swala la kawaida kwa sababu amekuwa akiongelea tangu akiwa mtoto.

Hamisa anasema kuwa hata akitoka shule alikuwa kunyooshewa sana yeye vidole kuliko watoto wengine wote na alipokuwa akimuuliza mam ayake alikuwa akimjibu ni kutokana na utofauti wake aliopewa na Mungu ndio uliomfanya awe hivyo.

download latest music    

Hamisa anasema kuwa hakuwa anajibizana na watu tangu akiwa mtoto na hata sasa ni kutokana na malezi yale aliyoyapata kutoka kwa mama yake na maneno mazuri ndio yanayoendelea kumpa moyo wa kufanikiwa zaidi nakujikuta akifanikiwa kila siku.

nadhani kila mtu ana moyo na kwa upand wangu pia ni hivyo hivyo kila kukicha likija jipya unakuwa tu unasema na leo hili tena .hii ni kwa sababu nimekuwa na moyo mgumu kwa sababu tangu niko nasoma kablwa isjakuwa maarufu nilikuwa nasemwa pia.

na nilikuwa namuuliza mamangu kwa nini nikipita kutoka shule ninaongelewa tu yaani,lakini mamangu aliniambia ni kwa sababu nina kitu special na ndio maana ninaongelewa kuliko watoto wengine.lakini pia ni kutokana na moyo wa mtu na vile mtu ulivyolelewa.

Siku za hapo nyuma kidogo mama wa mwanadada Hamisa aliwahi kunakiriwa akisema kuwa hata Dunia imfanye nini lakini hatokaa aache kumsapoti mtoto wake Hamisa kwa sababu ndio mtoto wake wa pekee.

Pamoja na yote anayopitia na kutukanwa kwa hamisa baba yake ameonekana kuwa mstari wa  mbele kumsapoti na kumkingia kifua na hata kusimama mbele za watu na kusema anajivunia mtoto wake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.