Tausi Aelezea Masikitiko Yake Baada ya Kumpoteza Mzee Majuto

Msanii wa maigizo, filamu na vichekesho  nchini Tausi Mdegela  alikuwa akionekana moja ya watu waliokuwa wakionekana kulia na kuumia sana siku ya  msiba wa Mzee Majuto.Hata hivyo baada ya kuchunguza na kumhoji mwenyewe pia alikiri kuwa mzee majuto alikuwa baba yake wa hiari ambae pia ndie aliemfundisha sanaa na kumfanya awe hapa alipo.

Tausi anasema kuwa Mzee Majuto alikuwa kama baba yake mzazi kwa sababu ndie aliemlea na amekuwa akikaa kwake kwa muda mrefu sana kama mtoto wake wa kumlea mpaka kumfundisha sana na kuanza kujitegemea na ndoto kubwa ya mzee ilikuwa ni kumuona akifanikiwa na kufika mbali katika sana.

download latest music    

mimi hapa naumia sana kwa uchungu kwa sababu ya kumpotea baba yangu ambae kwa muda wote amekuwa akinifundisha sanaa na amekuwa akiaka kuniona kuwa nina fika mbali, na pia kila siku alikuwa akitaka kujua hali yangu kama mwanae.

Tausi pia ansema kuwa kabla mzee majuto hajafariki kua mtu alimpigia simu kumwambia kuwa mzee alikuwa anamwita na alikwenda kumuona na kumsikilia kabla hajakata roho.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.