Tazama Picha na Video Za Lulu Akiwa Mahakamani Kwaajili Ya Kesi Ya Kanumba

Msanii wa bongo movie Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ amewasili leo mahakama kuu ya Tanzania kwaajili ya kuanza kusikilizwa kwa kesi yake ya kumuua bila kukusudia muigizaji wa bongo Movie marehemu Steven Kanumba.

Kesi ya Lulu imeanzwa kusikilizwa leo kwenye mahakama kuu ya Tanzania amewasili mahakamani hapo leo asubuhi akiwa ameambatana na mama yake Lucresia Kalugila. Huku marafiki wa karibu wa Lulu kama Muna Mapenzi akiwepo pia.

download latest music    

Mapema wiki hii iliwekwa wazi kuwa kesi ya Lulu iliyokuwa kimya kwa miaka kadhaa sasa itaanza kusikilizwa Alhamisi tarehe 19 kwenye mahakama ya kanda ya Dar es Salaam.

Hizi ni video zinazomuonyesha Lulu akiwasili Mahakamani leo asubuhi

 

 

Baada ya kesi ya lulu kusikilizwa kwa masaa kadhaa ambapo shahidi mmoja alitoa ushahidi kesi ilitangazwa kuendelea kisomwa siku ya kesho. Lulu alionekana akiondoka maeneo ya mahakama kwa kupanda gari la mwanasheria wake Peter Kibatala.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.