TCRA Yazifungia Nyimbo 13, Diamond na Nay wa Mitego Walizwa Zaidi

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imefungia kuchezwa kwa nyimbo kumi na tatu za wasanii mbali mbali huku Nay wa Mitego na Diamond wakiwa na zaidi ya nyimbo moja kwenye orodha hiyo.

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha kuchezwa kwa nyimbo 13 zisizokuwa na maadili zikiwemo mbili za Msanii Diamond Platnumz.

download latest music    

TCRA waliandika maelezo haya na kuorodhesha nyimbo hizo:

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania imepokea nyimbo zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Nyimbo hizo zilitolewa na wasanii na kusambazwa katika vyombo mbalimbali vya utangazaji na mitandao ya kijamii. Nyimbo hizo zina maudhui ambayo ni kinyume na maadili na kanuni za huduma za utangazaji (maudhui) 2005”.

Hii ndio listi kamili ya nyimbo zilizotolewa na Mamlaka ya mawasiliano;

 

Mamlaka ya mawasiliano imetuma kopi hiyo ya barua kwa vyombo vyote vya habari na kuvitaka kusitisha kucheza nyimbo hizo mara moja na pia vyombo hivyo vimehaidi kuchukua hatua kali za kisheria kwa chombo chochote kitaendelea kucheza nyimbo hizo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.