Team-Wema Wakiri Kumchoka Wema Sepetu

Mashabiki wanaojitolea kum-support  wema sepetu wamekuja juu na kumtupilia mbali msanii huyo, Wema ni mwanadada wa bongo movies ambae  ana mashabiki wengi sana katika mitandao ya kijamii uhusani instagram, wakiandika katika ukurasa  wa instagram moja ya viongozi wa team hiyo anaijiita wemaselfies, amefunguka na kusema kuwa wamechoka tabia za madame wao.

Mashabiki hao wamelalalmika na kusema kuwa kwa muda mrefu sana Wema amekuwa kimya hana kazi yoyote mjini, hatoi hata movie yoyote kila siku kuahidi lakini hakuna kinachokamilika, wakatolea mfano wa movie mojawapo ambayo Wema Sepetu aliitangaza kwa muda mrefu aliomshirikisha Van Vicker lakini mpaka leo movie hiyo haijatoka na mashabiki wakiwa wamekaa wanaihusibiri.

download latest music    

Hata hivyo team hiyo inalalamika na kusema kuwa kwa muda  Wema amekuwa akifanya mambo ya aibu lakini wamekuwa wakimsapoti sana wala hawalipwi chochote zaidi ya mapenzi kwa msanii huyo lakini kitu cha kushangaza ni kwamba wanapofanya jukumu la kumwambia wanaishia kugombana na msanii huyo.

Wakimtolea mfano na kumfananisha na Huddah the boss kutoka Uganda, team hiyo inasema kuwa Wema amekuwa mtu wa kuanzisha biashara lakini zinakuwa zinakufa kwa mfano wa biashara yake ya lipstick haijulikani mpaka leo iko wapi wakati watu kama  Huddah wameanza hivi juzijuzi lakini sasa hivi wako mbali na biashara zao.

Mashabiki wa Wema wamekuwa watu wa kukata tamaa kutokana na tabia ya Wema kuendelea kujipendekeza kwa Wasafi na boss wao Diamond wakati mapenzi yao yalishaisha siku nyigi ingawa yeye mwenyewe anasema kuwa hana kinyongo na Diamond, kitu ambacho Team wema wanatafsiri ni kama kumbembeleza Diamond na familia yake, wakamtolea mfano na mwanadada Penny ambae pia alikuwa ni mpenzi wa Diamond lakina alipoachana nae aliamua kufunga milango yote ya mawasiliano na kuwa karibu na msanii huyo.

Haya yote yatakuwa yamesababishwa na tabia ya msanii huyo kuwa anafanya mambo ya aibu huku team zake wakimtetea huku wakijua kuwa mambo mengine sio sahihi kwa msanii wao kuyafanya, hivi karibuni kuna baadhi ya picha zilizosambaa kwa zaidi ya awamu mbili tofauti zilionyesha picha za Wema akiwa faragha na mwanaume.Lakini pia kumekuwa na tetesi kuwa mwanadada huyo kuwa bado na mahusiano na msanii Diamond ingawa yeye mwenyewe alikanusha tetesi hizo.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.