Tetesi za Ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja Zazidi Kushangaza Wengi

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya, amezidi kushika vichwa vya habari mwishoni mwa wiki hii baada ya habari kuenea kwa kasi kuwa anaolewa na mwanamuziki wa bongo fleva Dogo Janja.

Tetesi za Uwoya na Dogo Janja zimekuwa zikisambaa kwa muda sasa huku kila mmoja akikataa kuwa na uhusiano na mwenzie. Siku ya Ijumaa oktoba 28 taarifa zilienea kuwa Uwoya anaolewa lakini bwana harusi hakuwekwa wazi kuwa ni nani na inasemekana kuwa ndoa hiyo ilifanyika kwa siri kubwa sana kwani habari za chini chini zinadai wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hiyo hawakuruhusiwa hata kupiga picha na wengine walilazimishwa kufuta picha hizo.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya aliweka wazi kuwa amebadilisha dini na kuwa muislamu na kubadili jina na kuitwa Sheila. Uwoya aliweka picha zake za harusi lakini picha za bwana harusi hazikuonekana.

Habari za Dogo Janja na Uwoya kufunga ndoa ziliwashangaza wengi kutokana na tofauti kubwa ya kiumri iliyopo baina yao. Siku ya jumamosi mastaa mbali mbali ambao ni marafiki wa Dogo Janja na Uwoya waliwapongeza wawili hao kwa kufunga ndoa, mastaa hao ni kama vile Zamaradi, Madee,Shetta na wengineo.

Picha zilisambaa pia zikimuonyesha Dogo Janja akiwa amevaa khanzu huku wengi wakidai kuwa ametoka kuoa.

Baadhi ya habari pia iliyosambaa ni kuwa Uwoya ameolewa na kigogo ambaye hataki ajulikane hivyo kamtumia Dogo Janja kama kuuwa soo jambo ambalo binafsi sidhani kuwa ni kweli kwani ukiangalia kwenye sehemu zote ambazo Uwoya amepongezwa kwa kuolewa na Dogo Janja hakuna hata sehemu moja aliyokataa kuwa mumewe siyo Dogo Janja.

Kama kweli Uwoya atakuwa ameolewa na Dogo Janja basi atakuwa amedhihirisha ule usemi usemao kuwa umri si kitu chochote mbele ya mapenzi kuwa mapenzi hayachagui. Pia ifahamike kuwa sababu kubwa ya Irene kubadilisha dini na kuwa muislamu ni kwa sababu kisheria na kidini ni mke wa mtu kwani ameolewa ndoa ya kanisani na mumewe wa zamani na baba wa mtoto wake Kataut Ndikumana hivyo asingeruhusiwa kuolewa tena kanisani hicvyo akafikia uamuzi wa kubadili dini.

Je nini maoni yako unadhani Uwoya na Dogo Janja wameoana tafadhali tiririrka maoni yako hapo chini.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.