Thea Apewa Ruksa Ya Kuolewa na Mumewe

Muigizaji wa Bongo movie Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea amepewa ruksa ya Kuolewa Tena na mume wake Michael Sangu ‘Mike’ baada ya kutangaza nia ya kutaka ndoa.

Mike na Thea walifunga ndoa miaka kadhaa iliyopita lakini baada ya kushindwana kukaa kwenye ndoa na kuachana Thea alitangaza kuwa anataka Kuolewa na mwanaume mwingine jambo ambalo mume wake Mike hana tatizo nalo.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mike amesema Thea ana uhuru hata wa kuolewa au kuzaa na mwa­naume yeyote anayemtaka kwani yuko huru hakuna sheria yoyote inayo­mbana kwa kuwa wakati wanafunga ndoa katika Kanisa Katoliki, walifunga ya mseto hivyo muigizaji huyo akawa anaendelea kusali kwenye kanisa la kilokole alikokuwa tangu mwanzo.

Thea yuko huru kuolewa au kuzaa hata na wanaume kumi maana hakuna kinachomzuia, shida iko kwangu maana dini ya Katoliki inatambua ndoa moja tu ambayo nili­funga naye na hatujawahi kuibatilisha”.

Kwenye mahojiano na Global Publishers wiki chache zilizopita Thea alitangaza nia ya Kuolewa baada ya kupata mwanaume mwingine.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.