Thea Atoa Pongezi Zake kwa Makonda , Ni Baada ya Kampeni ya Kusaidia Wanawake

Msanii wa bongo movies Ndumbaye Misayo maarufu kama Thea ameandika ujumbe mrefu kwa ajili ya kumpongeza Mh Paul Makonda baada ya kuanzisha kampeni ya kusaidia wanawake ambao wametelekezwa na wanaume zao na kuwaachia watoto kulea peke yao.

Thea aliandika hivi kuhusu kampeni hiyo ya Mh Paul:

download latest music    

kwanza nimpogeze mheshimiwa paul makonda kwa kujitolea na kulikumbuka kundi hili la wanawake waliojitokezwa, kwakweli tatioz hili ni kubwa sana  n kumuachia Mh Makonda peke yake haitwezekana kwa sababu tatizo sio kwa dar peke yake bali ni Tanzania nzima.

niombe wadau wa maendeleo ya wanawake tanznia kutafuta suluhu ambayo ni endelevu kwa tatizo hili.upo ukatili unaotokea kama ajali lakini ukatili huu mwingi kwa wanawak na wasichana utokana na umaskini.

wanawake hawa waliojitokeza leo inamaanisha kuwa hawajaweza kumudu hata yake mahitaji ya msingi nitoe wito kwa wanawake na wadau wengine kumuunga mkono Mh Paul Makonda ili kuweza pia kuwakwamua wanawake hawa kiuchumi.

Tuwasaidie wanawake hawa kuwa na uchumi imara kwa sababu sio wanaume wote wanakataa kutoa matunzo kwa makusudi, wengine wamekuwa wakiyumba.

Hata hivyo kutokana na kampeni hiikila mtu amekuwa na muonekano tofauti kwa sababu wapo wanaosapoti na pia wapo wanaosema zoezi haliwezi kumaliza tatizo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.