Tiko Awasahauri Wasanii wa Bongo Kuwa Watiifu kwa Serikali.

Msanii wa bongo movies nchini Tiko Hasssan amefunguka na kuwataka wasanii wa bongo kuwa watiifu pale wanapoambiwa kutekeleza jambo na serikali ili wasiweze kupatwa na madhara maengine yanayoweza kutokea baada ya kukiuka sheria hizo.

Tiko amesema kuwa kuna baadhi ya wasanii unakuta wanahitajika kufika mahali flani na mamalaka inayohusiana na sanaa lakini wanakiuka maagizo hayo alafu ukifika muda wa kuipoea adhabu anakuwa mkali na wa kuanza kulalamika wakati picdi wanapokuwa wanaitwa inakuwa ni kwa manufaa ya kazi zao wenyewe za sanaa .

download latest music    

Akitolea mfano kutoka kwa wasanii wa muziki, Tiko anasema kuwa serikali kupitia Baraza la habari, sanaa , tamaduni na michezo wamekuwa wakiwaita wasanii ili kukaaa nao chini kuzungumza nao kuhusu marekebisho ya kazi zao hasa wasanii wa muziki lakini wanakuwa wanapuuzia na kushinwa kufika kwa kudharau.

Jamani mastaa tunatakiwa kuheshimu serikali , aple unapoitwa  wito unatakiwa kutii wito huo. kwa sababu hiyo ndo inayosaidia katika kazi za sanaa.- Alifunguka Tiko Hassan alipokuwa akiongea na  za moto moto news.

Haya yote yanakuja baada ya wki moja iliyopita wasanii wengine kukumbwa na sakata la kufungiwa kwa kazi zao na serikali kwa madai ya kwenda kinyume na maadili ya Tanzania katika utoaji wa kazi zao na mavazi yao kitu ambacho kimewaumiza wasanii wengi huku baraza la sanaa likisema kuwa wasanii hao wamekuwa wakipuuzia wito na barua za mazungumzo wanazotumiwa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.