Timbulo Adai Hataki Ukaribu na Wasanii Wenzake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Timbulo amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye ni msanii ambaye hataki sana ukaribu na Wasanii Wenzake.

Timbulo anayefanya vyema na kibao chake cha ‘Sangoma’ amefunguka na kueleza sababu ambazo zinamfanya kutokuwa na ukaribu na Wasanii Wenzake wa Bongo fleva.

download latest music    

Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews cha EATV, Timbulo amekiri kuwa haonekani sana na wasanii wenzake akijichanganya kwa sababu hajawahi kupata mwaliko kutoka kwa wasanii hao.

Sionekani Kwenye events kama hizo za wasanii wengine kwa sababu sijaalikwa ila ningealikwa ningeenda na labda sijaalikwa kwa sababu mimi sijawahi kuwaalika lakini mimi utaniona Kwenye misiba ya wasanii wengine maana hakuna mialiko”.

Lakini pia Timbulo ameweka wazi kuwa hana ukaribu na Wasanii kwa sababu hataki mazoea sana na anataka kufanya kazi Kwenye sanaa kuliko mambo mengine Lakini pia amedai kuwa hawezi kuwa na ukaribu na wapinzani wake ambao ni wasanii wenzake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.