Timbulo Amwaga Povu Kwa Wanaombeza Kwa Kumiliki Gari Aina Ya IST

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Timbulo amefunguka na kumwaga povu kwa mashabiki na wadau wote ambao wamekuwa wakimbeza baada ya kuona mafanikio yake yaliyotokana na muziki.

Timbulo amedai kusikitishwa na baadhi ya wadau wa muziki nchini Tanzania ambao wameonekana kushangazwa na  mafanikio yake baada ya kusikia kwamba kuna watu wanaona hastahili kumiliki vitu kama nyumba na magari.

download latest music    

Timbulo ambaye amekuwa akionekana mara kwa mara akianika mali zake Kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwemo nyumba na magari amedai anajiona anastahili kumiliki mali kama wasanii wengine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Timbulo amedai wasanii wa Bongo fleva  wanastahili kuwa na mali nyingi sio watu kushangaa yeye kumiliki gari kama IST.

Tunaona namna gani ambavyo tunajaribu kurudishana nyuma kwa sababu ukitazama namna ambavyo nimepambana mpaka kufikia leo, toka 2005 mpaka leo 2018, so ukiniambia leo si shahili kuwa hata na maisha ambayo naonekana nayo nakuwa roho inaniuma sana kwa sababu naona jinsi gani tunarudisha nyuma.

Sisi kama wasanii wa Tanzania tunastahili kuwa matajiri, tumefanya kazi kubwa sana, wenzetu mbele ngoma moja inabadili maisha yao, why mimi na ngoma zaidi ya 20 halafu mtu anashangaa mimi kulimiki IST”.

Siku za nyuma Timbulo ameshawahi kukumbwa na skendo ya Kuazima magari na kupiga picha ili kuonyesha kama ya kwake Kwenye mitandao tetesi alizozikana.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.