Timbulo Aomba Radhi Mashabiki, ni Baada ya Kukataa Kutoa Msaada.

Msanii wa bongo fleva Timbulo awaomba radhi mashabiki na watanzania kwa ujumla baada ya wiki iliyopita kupigiwa simu na watangazaji wa kipindi cha Shilawadu na kumtaka atoe msaada kwa moja ya vijana ambao alishawahi kufanya nao kazi katika muziki wake anaejulikana kama Emma ambae ni dancer katika video mbalimbali.

Mcheza shoo huyo amabe hali yake inaonekana kuwa mbaya sana kiafya amethibitisha kuumwa kwa muda mrefu sasa akisumbuliwa na kifua kikuu na kwamba amekuwa akinywa dawa ambazo inahitajika ela nyingi kwa ajili ya kununua vyakula na ukitegemea yeye ndie aliyekuwa baba wa familia yake.

download latest music    

Emaa anasema kuwa amefanya kazi na wasanii wengi akiwemo Alikiba ambae ndie amekuwa msanii anaemsaidia na kumpa ela mara kwa mara kwa ajili ya matibabu lakini hawa wengine wamekuwa wakimkwepesha na hata kumkatia simu zake.

Wakiwa hapo hapo kwa mgonjwa Soudy Brown na Qwisah waliamua kumpigia Timbulo ili kumuelezea hali ya kijana huyo ndipo msanii huyo alikuwa akiwajibu vibaya na kukata simu, lakini msanii huyo ameamua kuja na kuomba msamaha na kukubali kumsaidia kijana mwenzake.

Unajua emma mimi nimdogo wangu ukiachana na kufanya nae kazi za sanaa kwaio sikupaswa kutangazwa kila kitu kuhusu kumtembelea,kwa kuwa tunapaswa kushare kwa misaada zaid naomba mnisamehe kwa niliemkwaza  au kuguswa kwa namna yoyote ile , kwa sasa nimesafiri baada ya pasaka nitarudi na nitaenda kumuona mdogo wangu, nawapongezz sana shilawadu , wakati mwingine tunaonaga kama jamaa simu zao zinakuwa za umbea au udaku kumbe zingine zinakuwa na maana, kwasasa naomba tumchangie emma kwa kitu chochote kama una mia, mia tano elfu tano  kwa namba yake lakini pia unaweza kumpigia na kumpa pole.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.