Tip Top Haijafa Ila Majukumu Ndio Mengi- Dogo Janja

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Dogo Janja ameibuka na kuongelea suala la kundi la Tip Top Connection kuvunjika ambapo amedai halijavunjika bali kila msanii ana majukumu mengine.

Kundi kwa Tip Top Connection liliwahi kuvuma sana na kufanya vyema sana miaka ya nyuma na liliundwa na wasanii kama Madee, Kassim Mganga, Keysha, Dogo Janja na wengineo.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Dogo Janja amesema kuwa sio kweli kuwa kundi hilo limekufa kutokana na kwamba hawatoi wimbo wa pamoja bali majukumu mengine na muda vimewatenganisha.

Tip Top ipo pale pale, umri na majukumu sio watu tena wa kukusanyana masikani tena ndio kitu ambacho watu wanakuwa wanapishana sana lakini Tip Top ipo na inafanya.

Watu wanazungumza kwa sababu hakuna wimbo wa kundi nahisi ndio chanzo cha watu kuzungumza hivyo”.

Wasanii ambao walikuwa wanaunda kundi hilo wamesambaratika huku kila msanii akiwa anafanya muziki wake ingawa wamekuwa wakionekana pamoja Kwenye matukio mbali mbali pamoja kama Kwenye Harusi ya Dogo Janja.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.