Tumbo Kubwa La Thea Lazua Utata

Muigizaji mkongwe wa filamu za Bongo movie Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea alizua gumzo mbele ya hadhara Baada ya kuonekana kuwa na tumbo kubwa kupitiliza.

Kutokana na kitambi hicho mara moja kuna taarifa zilisambaa kwamba huenda mwanamama huyo ni mjamzito na watu wengi ndiyo maana tumbo limemtoka hivyo au kama ni kuridhika na maisha basi ameridhika kwelikweli.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers  na kuulizwa kuhusiana na madai kwamba ni mjamzito au laa, Thea alikuwa na haya ya kusema:

Jamani sina ujauzito, hili tumbo ni kwamba nimenenepa tu, yaani nimeridhika na maisha ninayoishi lakini kama watu Wananichuria haina shida kwa sababu kuzaa ni jambo jema sana.”

Mashabiki wengi walionekana kuuponda muonekano wa Thea na kumkosoa kwa kujiachia na kunenepeana tu na kupoteza mvuto Wake Kama msanii.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.