Tunda Akiri Kuogopa Kumuongelea Tena Zari

Mrembo Tunda Sebastian ambaye ni Video queen maarufu amefunguka na kusema hatokaa kumuongela Zari wala kuvunjika kwa penzi la Diamond na Wema.

Tunda amedai amefikia uamuzi huo baada ya kukiri kuoga mvua ya matusi kila mara akifungua mdomo wake kuongelea jambo lolote linalomuhusu Zari amekuwa akiishia kuoga mvua ya matusi kutoka kwa Watanzania.

download latest music    

Tunda alipata umaarufu zaidi mwezi uliopita baada ya kupatwa na skendo ya kutoka kimapenzi na Diamond ambaye kwa kipindi hiko alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mzazi mwenzake Zari the Bosslady.

Kwenye Interview aliyofanya na Global Publishers Tunda alifunguka na kusema kuwa amefikia uamuzi wa kutokaa na kumzungumzia tena Zari kwani chochote kile anachokizungumza watu wataanza kumshushia mvua ya matusi na familia yake haipendi kuoana anatukanwa vile.

Kwenye mahojiano hayo Tunda ameongea haya:

Mimi kuhusu Zari au sijui ishu zao za kuachana kwao na Diamond au kitu chochote kinachohusiana na mambo yao sitaki kabisa kuzungumzia maana wengine sisi Damu zetu ni kama za kunguni nikisungumza chochote itakuwa ni shida tupo”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.