Tunda Amesema Haya Kuhusu Uhusiano Wake na Diamond Pamoja na Zari

Video queen maarufu Bongo Tunda amefunguk tena kuhusiana na uhusiano aliokuwa nao na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari the boss lady.

Wiki chache zilizopita Tunda amekuwa akitawala vichwa vya habari mbali mbali katika mitandao huku mara zote akihisishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond lakini mara kwa mara amekuwa akikataa na kudai kuwa yeye ni shabiki wake tu na sivinginevyo.

download latest music    

Kwenye interview aliyofanya na Millard Ayo Tv, Tunda amefunguka na kusema yeye yupo karibu na Diamond kama shabiki lakini hana uhusiano naye lakini Zari hajawahi kuwasiliana naye wala kumtafuta kwa sababu hana cha kimwambia.

Narudia tena Mimi nahisi nasemwa sana kuwa na mahusiano na Diamond kwa sababu niko free kuweka wazi kwamba Diamond ndiye msanii ninaye mkubali sana kwa hapa Bongo tofauti na msanii mwingine sijawahi kuweka wazi nahisi ndio inapelekea watu kufikiria hayo lakini yule sio mpenzi wangu ni mtu tu ambaye namuheshimu   na yeye mwenyewe anaelewa support yangu kwake lakini sio mapenzi”.

Kwenye mahojiano hayo Tunda aliulizwa endapo ameshawahi kukutana na Zari au kumtafuta ili azungumze naye na jibu alilotoa kwa kung’aka ni amtafute Zari ili amwambie nini maana yeye anamkubali Diamond na wala sio Zari.

Tunda pia amefunguka na kudai kuwa hivi sasa yuko busy na kazi zake za kisanaa ambapo ameshirikishwa kwenye video mpya ya Barnaba.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.