Tunda Amuomba Msamaha Aunty Ezekiel Baada Ya Kumtukana Mtoto Wake

Video vixen na Socialite maarufu Tunda Sebastian amefunguka na kumuomba radhi msanii wa Bongo movie Aunty Ezekiel baada ya kumtukana mtoto wake na Mose Iyobo, Cookie.

Miezi michache iliyopita kulizuka bonge valangati baada ya Aunty Ezekiel kumuashia dude Tunda ambapo alienda kwenye ukurasa wake instagram na kumdai pesa yake aliyomkopesha pombe dukani kwake.

download latest music    

Baada ya hapo walianza kurushiana maneno ya kejeli na matusi hata Tunda alifikia hatua ya kumtukana mtoto wa Aunty Ezekiel ambapo alimuita mtoto wake kuwa ni mtoto mbaya dunia nzima.

Wikiendi iliyopita Tunda amemuomba msamaha Aunty Ezekiel kwa kumtukania mtoto wake na kudai kuwa zilikuwa ni hasira tu na hakupanga kumtukana mtoto wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tunda alimuandikia Aunty ujumbe huu:

 

Kwa kipindi kirefu Kumekuwa na tetesi kuwa Tunda ni mjamzito na alithibitisha kuwa ni mjamzito kwa kuandika “Naomba msamaha kama mwanamke ambaye nitaitwa mama pia soon”. 

Kwa habari za chini ya kapeti zinadai kuwa ujauzito huo ni wa miezi mitatu na inasemekana kuwa baba wa mtoto huyo ni mtangazaji za Clouds Tv Casto Dickson ambaye ni Baba mtoto wa Munalove ambaye ni rafiki wa Tunda.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.