Tunda Awapa Ujumbe Mzito Wapenzi Wake Wote Wa Zamani

Model na video vixen maarufu Bongo, Tunda Sebastian ametoa ujumbe mzito kwa wapenzi wake wa zamani (ma-ex) na kuwaambia kuwa watamkumbuka tu.

Ingawa hajamtaja mwanaume yoyote kwa jina lakini Tunda alipata umaarufu zaidi hivi karibuni baada ya skendo yake na Diamond na tetesi zilienea kuwa amekuwa mchepuko wa staa huyo wa Bongo fleva kwa muda mrefu hadi alifikia hatua ya kumbebea mimba.

download latest music    

Baadhi ya wanaume ambao Tunda ameshawahi kubanjuka nao ambao ni mastaa ni pamoja na Diamond, Mfanyabiashara maarufu Kinje, na wasanii wa Bongo fleva Young Dee na Abdu Kiba.

Tunda alitumia ukurasa wake wa Instagram kufikisha ujumbe huo kwa wapenzi wake wa zamani ambapo amewaambia Maex wake  kuwa wakimuona anataka wajue walichokipoteza, wajutie kwa kumpoteza yeye na wajue kuwa kamwe hawatampata Tena.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe huo uliosindikizwa na picha:

Dear Ex….when you see me, i want you to recognize what you have lost, and realize what your never getting back”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.