Tuzo ni Kipimo Kikubwa Cha Kazi Ya Msanii:-Joh Makini

Msanii kutoka katika kundi la weusi , joh makini amefunguka na kusema kuwa kutokuwepo kwa tuzo nchin tanzania kuna didimiza sana muziki wa tanzania kwa sababu hakuna kipimo halisi cha ukubwa wa kazi za wasanii.

Joh makini anasema kuwa tuoz inakuwa inampa msanii hamasa ya kufanya kazi kwa umakini zaidi ili aweze kupata tuzo lakini ndani yake anakuwa akifanya muziki mzuri ambao ni faidia kwake na kwa mashabiki pia.

download latest music    

joh Makini anaifananisha tuzo na nafasi ya mwanafunzi anapokuwa shule akisoma kwa bidii ili akae katika nafasi nzuri huku akijua kabisa kuwa kuna zawadi itakuja kwa ajili yake.

Tuzo ni kitu cha msingi na kipimo kikubwa sana kwa nafasi ya msanii kujua ukubwa wa kazi yake,kwa sisi weusi tunajua kabisa kuwa sisi ni wakali na tumekuwa tukifanya vitu vikubwa na vya kushangaza watu

Kwa muda sasaTanzania kumekuwa hakuna tuzo, kutokana na figizu za hapa na pale huku wasanii wengi wakilalamika kuonewa katika tuzo hizo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.