Uchunguzi uliofanywa kwa mkojo wa Wema Sepetu unashangaza mahakama

Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilitoa majibu kuhusu uchunguzi uliofanywa kwa mkojo wa Wema Sepetu. Mrembo huyo na wenzake Angelina Msigwa (21) na Matrida Abbas (16) walishtakiwa kwa utumzi wa bangi, walishikwa na msokoto mmoja wa bangi mapema Februari mwaka huu.

Jana kesi ya Wema Sepetu inayoendelea katika Mahakama ya Kisutu ilichukua mkondo mpya hapo jana baada ya ripoti kutoka kwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

download latest music    
Wema Sepetu akitoka Mahakamani

Elias Mulima kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali akisoma ripoti ya uchunguzi uliofanywa kwa mkojo wa Wema Sepetu. Mulima aliambia Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba, kuwa ripoti hio ilidhibitisha kuwa chembechembe za bangi zilipatikana katika mkojo wa Wema Sepetu.

Wakili wa Wema – Peter Kibatala hata hivyo alisema ripoti hiyo kutoka kwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ulikua na upungufu mwingi wa kisheria.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Thomas Simba alihairisha kesi hio ya Wema Sepetu hadi Agosti 4, mwaka huu.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere