Ugonjwa Uliomuua Mtoto Patrick Wabainika

Siku ya Jumanne usiku mtoto wa Muna aliyekuwa anaitwa Patrick aliyekuwa na miaka 8 aliaga dunia hospitalini alipokuwa anatibiwa Nairobi nchini Kenya.

Global Publishers wanaripoti kuwa katika harakati za kutaka kujua nini hasa kilimuua mtoto huyo walianza kuongea na Muna ambaye yupo nchini Kenya kwa hivi sasa ambapo alifunguka:

download latest music    

Kinachomsumbua mwanangu ni uvimbe kwenye ubongo na hajaamka kwa siku sita huku akiwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum ‘ICU’ hivyo tunasubiri aamke ndipo madaktari waangalie kama watamfanyia operesheni au la“.

Muna alifunguka hayo kabla ya taarifa za Kifo chake.

Lakini pia Daktari ambaye amewahi kumtibu mtoto na yeye alifunguka kuhusu ugonjwa wa mtoto:

Dk Chale alisema uvimbe kwenye ubongo kitaalamu huitwa ‘Brain Tumour’ ambao unaweza kuwa wa kawaida au kansa na husababishwa na njia kuu mbili; moja ni ubongo wenyewe na pili kutokana na viungo vingine.

Katika njia ya kwanza ni kwamba inawezekana ugonjwa huu ukarithi kutoka kwa familia kama baba au mama amewahi kuwa na matatizo hayo basi lazima na wengine warithi. Sababu nyinginezo ambazo zinachangia ni maambukizi ya virusi wa ugonjwa huo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, sababu za kimazingira ambayo mtu anaishi, kemikali za viwandani, vipodozi, chakula, dawa na nyingine nyingi.

Katika njia ya pili ya viungo vingine hutokana na kama mtu ana kansa ya mapafu, kizazi, matiti, figo, tezi dume hizi huweza kusa babisha uvimbe kwenye ubongo. Dk Chale aliendelea kufafanua kuwa uvimbe kwenye ubongo kwa upande wa watoto mara nyingi huwa ni kansa na siyo wa kawaida ndiyo maana huua haraka sana na hawawezi kupona maana uvimbe huwa chini ya ubongo na siyo kwa juu kama inavyokuwa kwa watu wazima.

Mwenyezi Mungu aendelee kufika za roho ya marehemu mahala pema peponi Amina.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.