“Uhusiano Wangu Mpya Sio Kiki ni Mapenzi Ya Kweli”- Nisha

Muigizaji wa Bongo movie aliyegeukia sanaa ya Bongo fleva hivi karibuni Nisha Rajabu maarufu kama Nisha Bebe ameibuka na kuweka rekodi kuwa mzungu aliyeonekana naye hivi karibuni mpenzi wake wala sio kiki.

Siku za hivi karibuni Nisha alimuanika Mwanaume mwenye asili ya Kizungu na kuonyeshana naye mahaba kupitia ukurasa wake wa Instagram lakini ghafla ilisemekana mzungu yule tayari ana Mke wake na kuwa ni Nisha ilikuwa ni kiki ya wimbo mpya.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi Nisha aliweka wazi kuwa yule jamaa ni mpenzi wake na ameamua kujaribu kuwa na mzungu baada ya kusalitiwa na wanaume wa rangi nyingine zote:

Ndiyo yule ndio mpenzi wangu, Nimeamua kujaribu kwa Mzungu maana nilishakuwa na Waafrika na Wahindi lakini niliambulia maumivu”.

Lakini pia Nisha alikuja juu alipoulizwa kuhusu suala la mpenzi wake huyo kuwa na mke halali wa ndoa kabisa:

Walimwengu huwezi kuwakataza kuongea, kama wana ushahidi wa vyeti vyake vya ndoa waniletee.  Hii siyo kiki bali ni mpenzi wangu halisi, wamekuwa wakinisema kwamba nakuwa na wanaume wadogo lakini kwa sasa nimempata saizi yangu lakini cha kushangaza hata huyu wanamsema kwamba ni babu sijui hawa walimwengu wanataka nini/?“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.