Ujumbe Mzito Wa Steve Nyerere Kuelekea 40 Ya Mzee Majuto

Msanii wa filamu za Kibongo na mwanaharakati wa mambo ya siasa Steve Nyerere ametoa ujumbe mzito Ikiwa ni siku chache mpaka kufikia arobaini ya Msanii mkongwe Mzee Majuto tangu aage dunia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Steve Amewaasa watu kumkumbuka Mungu siku zote za maisha yao kutokana na ukweli kwamba siku zetu za kukaa duniani ni chache na zinahesabika.

download latest music    

Tupo kwenye mapito ya kidunia sana,tunaishi kama tuna mkataba na Mungu hatuna hofu na Mungu,Tunasahau muda wa kuishi duniani ni mchache sana.

Tunasahau Muda Wa Ufufuo Wa Milele Inategemea Na Yale Mazuri Uliyofanya Ukiwa  Hai, Fedha ,Cheo ,Ustaa ,Vyote Mapito Pokea  Sikiliza Kataa Maskini Anapendwa Kusikilizwa Hata Kama Utakataa Jambo Lake“.

Mzee Majuto aliaga dunia tarehe 7 August mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mrefu ambapo alilazwa kwa muda mrefu Muhimbili na hata kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.