Ujumbe wa Eddy Kenzo kwa Diamond baada ya Rayvanny kupata uteuzi wa BET award

Rayvanny ameteuliwa katika kitengo cha ‘Best International View’s Choices’ akiwa ni msanii pekee kutoka Afrika katika kitengo hicho.

Diamond na wasanii wengine wamekua wakiwarai mashabiki wao wampigie kura Rayvanny mbaka ashinde tuzo hilo. Walioteuliwa watatuzwa Jumapili hii tarehe 25 katika ukumbi wa Microsoft jijini Los Angeles, Marekani.

download latest music    

Eddy Kenzo aliweka picha ya Rayvanny kwa mtendao wa Instagram kuwaomba mashabiki wake wampigie kura Mtanzania huyo.

“Attention East Africa!!!!??? Our Brother @rayvanny needs our support by just commenting with #pickrayvanny on any picture of your choice on social media we need another #BET in eastAfrica asap 2015 and 2017 will be remembered ??? Alhamdulillah ?? congratulations #Tanzania Bless up @rayvanny #ipickrayvanny ????” Eddy Kenzo aliandika.

Mganda huyo amewahi kushinda tuzo la BET, alishinda tuzo hilo 2015 katika kitengo cha ‘Viewer’s Choice Best New International Artist’, kitengo sawa ambacho Rayvanny anawania mwaka huu.

Eddy Kenzo akionyesha tuzo la BET aliyoshinda 2015

Diamond Platnumz alimshukuru sana Eddy Kenzo kwa kumpigia upato Rayvanny kushinda tuzo hilo la BET.

“Kenzooooooooooo!!!!! ????” Diamond aliandika kwa comment.

Eddy Kenzo alimjibu na kumpongeza kwa kukuza talanta nchini Tanzania.

“@diamondplatnumz I see you my bro??? you are great?? thank you for showing us these talented yut of our generation may God reward you 100% blood???” aliandika Eddy Kenzo.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere