Ujumbe wa Jaydee kwa profesa Jay baada ya kufunga ndoa

Jaydee ambaye ni msanii wa zamani katika industry ya Bongo amemsifia Profesa Jay baada ya kufunga ndoa ya kifahari na mpenzi wake anayejulikana kama Grace.

download latest music    

Harusi hiyo iliyofanyika katika kanisa la koliki la Joseph, Dar Es Salam na baadae sherehe karika Mlimani city hall – huku wasanii wengi wakijitokeza kumpa support Profesa Jay.

Jaydee ambaye alikuwa miongoni mwa marafiki waliojitokeza alimpa pongezi Profesa Jay na mkewe hivi karibuni akizungumza na Planet Bongo ya EA Radio. Jaydee alisema,

“Kwanza nimpongeze Prof Jay kwa hatua aliyochukua, ni hatua nzuri katika maisha kwa sababu kwanza ni kuzaliwa, pili ni kuoa au kuolewa na ya tatu ni kufa, kwa hiyo hii ni harusi ya pili katika maisha yake nimpongeze sana kwa uamuzi alioufikia.”

Msanii huyu aliendelea kwa kusema,

“Nimtakie kila la kheri katika maisha yake ya ndoa yenye furaha na mafanikio. Professor kama kaka yangu na kama rafiki yangu ni mambo mengi tumepitia pamoja, tumeweza kusapotiana katika kazi na mambo mengine, kwa hiyo ni furaha kwangu, si kama msanii mwenzake bali kama mwanafamilia,”

Pongezi mingi kwa wapenzi hawa kutoka Ghafla Tanzania.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua