Ujumbe wa Wolper kwa Diamond yawasisimua watu mtandaoni

Muigizaji wa filamu ya Bongo Jacqueline Wolper ametuma ujumbe kwa Diamond ambaye anasherekea siku ya kuzaliwa kwake leo.

Mrembo huyo alimsifu sana Diamond kwa kuinua sanaa nchini Tanzania kwa kuwasaidia wasanii wengine kunawiri kimuziki.

download latest music    
Jacqueline Wolper na Diamond

Ujumbe wa Wolper kwa Diamond uliwasisimua watu wengi mtandaoni, soma ujumbe huo hapo chini:

“Natamani kila mtu ajue roho yako nzuri na mchango wako ktk nchi yetu na jinsi gani umeweza kuinua wengine tunaowajua na tusiowajua pia!kijana mdogo lkn umeweza kukubalika nje na ndani ya nchi,kiufupi jina lako linaendana na roho yako una moyo wa almasi plus dhahabu unajua kula na vipofu mpk vilema ndo maana Mungu anakufungulia ridhiki zako..Wewe ni zaidi ya Almasi buana,Endelea kutuburudisha na mziki mzuri baba Tee….Happy birthday to you baba Nillan..Sema nn birthday yako bado sana mpk mwezi wa kumi mbali kapicha nako kameshawishi alafu maneno yangu pia yata expire???Nweiiz Nimejisikia tu ndugu zangu,sio mbaya na nyie mkifunguka kwa mazuri yake bwana Ngote #myboss”

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere