Ukinileta Huyo Mtu Sasa hivi Nitafunga Ndoa:-mimi mars

Mwana dada Mimi Mars amefanya mahjiano na moja ya waandishi wa habari na kusema kuwa pamoja na kwamba kumekuwa na wimbi la wasanii wengi kwa sasa wanafunga ndoa lakini kwake yeye anaona bado muda kwa sababu anasubiri mtu mwenyewe wa kufung nae ndoa ajitokeze na ndio awaze kufunga ndoa.

Mimi Mars amabe alishawahi kusikika akisema kuwa mapenzi yamekuwa yakimuumiza sana anasema kuwa bado kwa sasa hajapata mtu wa kumuoa hataki kuwa na papara kwa sababu mapenzi yalishamuumiza.

download latest music    

Alipoulizwa mimi mars kuhusu lini na yeye atafunga ndoa kama ilivyo sasa kwa wasanii wengi kufunga ndoa aliwajibu hivi:-

bado kidogo kwanza tumsubitie huyo mtu afike na kisha ndo tuanze kujua tunafunga ndoa lini,kidogo si siku yoyote lakini kama utaniletea huyo mtu sasa hivi haina shida basi mapema.

Wasanii wengi wa bongo sasa hivi wameanza kujiingiza katika mjaukumu ya kifamilia kwa kufanikisha swala la zima la kuingia katika mhusiano na kufunga ndoa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.