Ukweli wa Mahusiano ya Zari na Maulidi Kitenge

Kuna Picha na video zinazomuonesha Kitenge akiwa nyumbani kwa Zari, zilisambaa usiku wa Jumapili iliyopita kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram na kuzua gumzo kwa wafuasi mbalimbali wa mitandao ya kijamii.

Kwenye video hizo, Kitenge alionekana akiwa na watoto wa Zari akichezacheza nao huku Zari akiwa bize jikoni kuandaa msosi. Kwenye baadhi ya vipande vya video hizo, mtangazaji huyo wa EFM amesikika akimsifia Zari kuwa ni msafi na anajua kupika.

download latest music    

Katika vipande vingine vilivyopo mitandaoni, Kitenge alisikika akiwauliza mashabiki wake kama mrembo huyo wa Kiganda anafaa kuolewa au la.

Nilete posa au nisilete?” alisikika Kitenge huku wafuasi wake mtandaoni wakimpa maoni tofautitofauti.

Kuna ambao walimwambia afanye kweli amuoe, kuna wengine wakamtaka amuache maana ataingia kwenye bifu zito na Diamond ambaye yupo kwenye harakati za mwishomwisho kurejesha penzi lake lililokuwa limevunjika.

Baada ya kusambaa sana kwa taarifa hizi gazeti la Amani liliamua kumtafuta maulid kitenge na kumuuliza kuhusu mahusiano yake na mwanadada Zari na hapo ndipo balaa lilipozidi kuwa kubwa kwa sababu Maulidi hakuonekana kusita kusema kuwa yeye na zari ni marafiki tu na alimualika nyumbani kwake kupata lunch kwa sababu yeye yupo afrika ya kusini kwa ajili ya matangazo ya mpira wa kombe la dunia.

Hata hivyo Maulidi aliulizwa kuhsu swala la nia yake ya kutaka kumuoa zari kama ambavyo imesambaa katika mitandao ya kijamii na Maulid alisema “miye ni muislamu na yeye ni muislamu na pia hajaolewa, hata pia ninachojua kuhusu mahusiano yake na diamond ni kwamba wameachana

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.