Umri Wa Zari Wazua Balaa Kwenye Mitandao Ya Kijamii

Umri wa mwanamama Zari Hassan ‘Zari The Bosslady’ umekuwa tena mjadala Kwenye mtandao wa kijamii baada ya kudaiwa kudanganya umri wakr hivi karibuni.

Wikienda iliyopita ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa wa kwa Zari na sherehe yake alienda kuifanya nchini Uingereza, London lakini inasemekana aliwekwa Kwenye mahojiano kwa masaa kadhaa na kisa kikitajwa ni umri wa Zari.

download latest music    

Inadaiwa kuwa umri wa Zari uliopo Kwenye Cheti cha kuzaliwa na uliopo kwenye passport ya kusafiria ni tofauti ambapo Zari amedai ana miaka 38 ikimaanisha amezaliwa mwaka 1980 lakini kuna taarifa zinadai amezaliwa 1978 na nyingine mwaka 1975.

Mange Kimambi Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa kitendo cha Zari kudanganya umri kumemletea matatizo kwani kuna uwezekano wa kuzuiliwa kuingia Uingereza kwa miaka mitatu.

Umri wa Zari imekuwa ukioeta utata kwa muda mrefu huku baadhi ya watu wakidai Zari hana miaka 38 Anayodai anayo jambo ambalo ameshawahi kulikataa siku za nyuma.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.