Upelele wa kesi ya kukutwa na bangi inayomkumba Wema Sepetu umekamilika

Wema Sepetu ako na kesi kujibu mahakamani baada ya kushikwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili vidogo vya bangi.

Mrembo huyo wa filamu za Bongo alishikwa na polisi Januari wakati polisi walianzisha msako kunasa wanaotumia dawa za kulevya.

download latest music    

Wema alizuiliwa katika kitua cha polisi jijini Dar es Salaam kwa siku sita kabla ya kupelekwa mahakamani kushtakiwa kwa kosa la kupatikana na bangi.

Wema aliachiliwa baada ya upande wa mashtaka kuomba mahakama muda kukamilisha upelelezi wa kesi yake ya kukutwa na bangi.

Wakili wa Serikali Helleni Mushi jana Mai tarehe mbili aliomba kesi hiyo kuhahirishwa tena na kupangwa tarehe ya kuanza kusikilizwa ili watuhumiwa waanze kusomewa maelezo ya awali.

Wema sasa atarudi Mahakamani hivi punde baada ya koti kuweka tarehe ambayo kesi yake itaskizwa. Mrembo huyo alishtakiwa pamoja na wafanyakazi wake wa ndani Angelina Msigwa (21) na Matrida Abas (16).

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere