Ushauri wa Muna kwa Wanawake Wenzie

Mwanadada Muna love ameamua kutoa ushauri wa bure kwa wanwake wenzie wanaobeba mimba  za baba wengine na kuwapa wanaume wengine wazilee mimba hizo eti kisa wanaume waliowapa mimba wamekataa mimba zao.

Akiongea katika Press Conference aliyoifanya leo nyumbani kwake, Muna alisema kuwa wakati wa mazishi aliongea na casto na walikubaliana kuwa wayamalize matatizo yao na kukubali maiti kufikia nyumbani kwa peter kwa sababu tu walikuwa hawataki kugombana  na ndugu na walitaka msiba huo upite lakini sio kwamba mtoto Patrick ni mtoto wa Peter.

download latest music    

Muna anasema  Casto alimwambia “mama pati mimi na wewe tunaujua ukweli ila huwezi kuwabadilisha watu,nimekosea kwa nafis yangu naomba unisamehe kwa sasa hivi tujifanye wajinga tu ili mtoto haifadhiwe kwa sababu kosa tulilokosea ni kuandika jina la mtoto na jina la baba mwingine.

Baada ya kuongea hivi muna nawashauri wanawake wengine na kusema “mimi leo nakiri kwa wanawake wenzangu kuwa hata kama mwanaume mkiwa na mapenzi kiasi gani na una mimba ya mwanaume mwingine usikubali kumpa akalea tu.

Hata hivyo uamuzi wa muna kuongea na waandishi umepokelewa tofauti sana na watu mbalimbali huku wengi wwakisema imekuwa mapema sana kwake kuongea na waandishi kutokana na msiba mkubwa uliompata.

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.