“Usiogope maneno ya watu” Diamond Platnumz amwambia Harmonize

Wikendi hii iliyopita, Diamond Platnumz, Harmonize na warembo wao walifika katika klabu maarufu ya Nairobi, B Club kuwatumbuiza mashabiki wao wa Kenya katika show iliyowavutia wengi.

Wakali hao wawili wanaaminika kuwa marafiki wa karibu waliwapa wengi kitu cha kuongea hasa baada ya kuonekana na warembo wao, Zari na mpenzi mpya wa Harmonize anayetambulika kama Sarah.

download latest music    

Hata hivyo Diamond Platnumz aliwashangaza wengi baada ya kumuandikia Harmonize ujumbe kupitia Instagram huku akimsihi asiogope maneno ya watu kwani wamepata fedha na mali ya kutosha kupitia muziki wao.

Tazama picha hiyo hapa;

https://instagram.com/p/BXMcjb7FSgD/

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua