Uwoya Afungukia Skendo Ya Kuwa na Danga Dubai

Muigizaji wa Bongo Movie Mrembo Irene Uwoya amefungukia skendo iliyomuandama Kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita baada ya kudaiwa kuenda Dubai kutanua na mwanaume mwingine.

Uwoya ambaye ameolewa na msanii wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja alidaiwa kuonekana Dubai akili bata na mwanaume mwingine ambaye alisemekana kuwa ni danga lake.

download latest music    

Global Publishers wanaripoti kuwa Uwoya na mume wake Dogo Janja hawana maelewano tena ndani ya ndoa yao hivyo mwanamama huyo alikwenda kupumzisha akili yake huko Dubai.

Baada ya tetesi hizo Gazeti la Ijumaa Wikienda lilifanya naye mahojiano kuhusiana na ishu hiyo ambapo alifunguka na kukataa tetesi hizo na kudai alienda Dubai kwa ajili ya mapumziko mwenyewe bila Mumewe sababu hawezi kwenda naye kila sehemu:

Jamani kwani kila sehemu ninatakiwa niwe naye? Hata kama nipo kikazi? Nilienda Dubai Kupumzika, tatizo Wabongo mtu akiamua kwenda sehemu nzuri, basi utasikia amelipiwa, kwa nini jamani? Tunapaswa kubadilika, nimetumia pesa zangu kujipa amani na furaha.

Baada ya kubanwa kuhusu njemba aliyewezesha safari ile badala ya mume wake, Uwoya alifunguka:

Ndiyo maana nikakuambia hatuwezi kuendelea kwa kufikiria kwamba mtu hawezi kufanya kitu mwenyewe mpaka alipiwe na mtu!“.

Baada ya Uwoya kusemekana kuwa Dubai na mtu mwingine mashabiki walimjia juu na kudai anafabya vile kwa sababu Mume wake Dogo Janja ni mdogo kwake hivyo anakuwa kama anamuonea.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.