Uwoya Athibitisha Kuwa Kwenye Mahusiano Mapya

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Irene Uwoya ameibuka na kukiri kuwa Hivi sasa yupo kwenye mahusiano mapya na mwanaume mwingine ambaye hajamtaja.

Uwoya ambaye aliachana na Mume Wake ndoa ambaye ni Msanii wa Bongo fleva Abdul Chande ‘Dogo Janja’ amesema Hivi sasa ana Mpenzi mwingine.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na waandishi w Habari kwenye sherehe za uzinduzi wa foundation ya msemaji wa Simba Haji Manara,  Irene Uwoya amesema kwamba ni kweli kwa sasa yupo kwenye mahusiano, na mpenzi wake huyo ni mfanyabiashara.

Ofcourse nipo kwenye mahusiano, yeye ni mfanyabiashara ila siwezi kuwatajia jina”.

Ingawa Uwoya amekataa kumuweka wazi Mpenzi Wake lakini kumekuwa na tetesi kwenye Mitandao ya kijamii kuwa mrembo huyo yupo kwenye mahusiano na mfanyabiashara ambaye ana mkwanja mrefu na ndio anamuweka mrembo huyo mjini kwa sasa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.