Uwoya Atiwa Mbaroni Baada Ya Kukutwa Anakunywa Baa Usiku Wa Manane

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Irene Uwoya na wasanii wenzake kama Tausi Mgedela, Idris Makupa ‘Kupa’, Hamis Changale ‘Mtanga walijikuta mikononi mwa polisi Mkoani Mbeya.

Wiki iliyopita kuna stori ilitrend kuwa Uwoya na Wasanii Wenzake walikamatwa mkoani Mbeya walikoenda kufanya shughuli za kijamii lakini kuna taarifa zilidai walikamatwa na sasa inadaiwa kuwa walikamatwa baa Usiku wa manane.

download latest music    

Global Publishers wanaripoti kuwa wasanii hao walikamatwa usiku wa Jumamosi iliyopita ya Septemba 22 kuamkia Septembea 23, mwaka huu baada ya kukutwa wakinywa pombe baa jijini Mbeya wakiwa wamevuka muda wa baa kufungwa. Kwa kawaida sheria zinaonesha kuwa baa inatakiwa kufunguliwa saa 10:00 jioni na kufungwa saa 5:00 usiku, lakini wao hawakujali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (RPC), Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Ulrich Matei amefunguka:

Walikamatwa na Polisi wa doria baada ya kukutwa baa wakiendelea na mambo yao wakati muda wa kufunga baa umepita. “Tuliwakamata na tulitaka wao ndiyo wawe mfano bora kwa jamii kwa sababu ni kioo cha jamii. “Lakini sikutaka kulikuza jambo hilo kwa sababu lilitokea wakati taifa lipo kwenye msiba mzito uliotokana na ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kule Ukerewe.

Hivyo niliona jambo hilo lisituondoe kwenye maombolezo, kwa hiyo tuliwapa elimu na kuwaachia, lakini liwe ni funzo kwa wengine. “Ni marufuku kunywa pombe muda wa kazi na ni marufuku kupitiliza muda wa kufunga baa.”

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.