Uwoya Atoa Vitisho Kwa mtu Anaedai ni Jirani Yake.

Mwanadada Irene Uwoya ametoa vitisho kupitian  ukurasa wake wa instagram baada ya kusema kuwa kuna jirani yake amekuwa akifatilia sana maisha yake wakati kwake yeye ni kitu cha kawaida sana.

Ingawa haijajulikana kama vitisho na majigambo hayo yanamlenga nani zaidi ya kusema kuwa ni jirani yake, Irene amekuwa na bifu na mume wake waliochana hivi karibuni  Dogo janja hivyo mashabiki wanahisi kuwa inawezekana madongo hayo yanakuwa yanamlenga ex wake huyo.

download latest music    

katika ukurasa wake wa instagram, Irene Uwoya aliandika “kuna jirani yangu anapata tabusana na maisha yangu,anaongea sana ooh magari sio yake,oooh hana pesa ohh anajidai sana,  na bado  mimi nataka nikwambie kitu  utapata tabu sana  kwa sababu uvionavyo ni rasharasha tu.”

Lakini pia irene anasema kuwa kwa kubwa zaidi watu hao wakae mkao wa kula kati  ya tarehe 18 hadi 22 kuna kitu kikubwa kitafanyika na kwamba waache kuhusisha maisha yake na maisha ya mtoto wa watu ambae yeye hajataka kumtaja kuwa ni nani.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.