Vanesaa Mdee Afunguka Kuogopa Kufunga Ndoa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amefunguka na kuweka wazi kuwa anaogopa sana kufunga ndoa licha ya kwamba umri Wake alionao unamruhusu kufanya hivyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Vee Money alisema licha ya kwamba ana umri wa miaka 30 kwa sasa, lakini hajawaza kuolewa kwa sababu anaogopa atabanwa na majukumu ya ndoa na kushindwa kufikia malengo aliyonayo.

download latest music    
Vanessa Na Mpenzi Wake Jux

Umri wangu umefikia wa kuingia kwenye ndoa, lakini siwezi kwani nina malengo makubwa ambayo bado sijayatimiza hadi sasa hivyo nahofia nikiingia kwenye ndoa kuwa nitabanwa na kushindwa kuyatimiza, maisha ni malengo hivyo siwezi kukurupuka tu, nikishayatimiza hayo malengo ndipo nitaingia kwenye ndoa“.

Vanessa amekuwa kwenye uhusiano wa miaka mingi na Mpenzi Wake ambaye pia ni Msanii wa Bongo fleva Juma Jux.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.