Vanessa Mdee Akumbwa na Skendo Ya Utapeli

Mwanamuziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee amejikuta katika wakati mgumu baada ya kunyoshewa vidole na kudaiwa kuwa ni tapeli baada ya watu waliouza albamu yake ya ‘Money Mondays’ kudai hawajaliowa.

Mwezi uliopita Vanessa aliachia albamu yake ya kwanza alioyoiita jina la Money Mondays. Albamu ambayo iliuzwa kwa njia zote yaani kidigitali kumaanisha kipitia mitandao mbali mbali ya kuuzia muziki Lakini pia kwa DVD yaani CD zilizouzwa mtaani.

download latest music    

Stori Hizi za kutapeli wauzaji wa albamu yake zimekuwa zikisikika chini chini lakini siku ya jana kwenye kipindi cha XXL ya Clouds Fm Soudy Brown aliongea na mwanadada aliyejitambulisha kama Jacky Tarimo aliyedai kuwa wamefanya kazi ya kuuza albamu hiyo kwa siku ishirini lakini wakiombwa walipwe wanakataa.

Kwenye mahojiano hayo mdada huyo alidai kuwa walikuwa wanataka  kufanya kazi mara mbili kwa wiki na kila siku ni shilingi elfu 15 na walifanya kazi kwa siku 15 lakini hawajaliowa hata senti mpaka muda huu.

Vanessa Mdee alipotafutwa ili kujibu tuhuma hizo hakupokea simu na meneja wa Vanessa anayeitwa Tahiya alikataa kujibu chochote kuhusu tuhuma hizi.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.