Vanessa Mdee Amesema Hana Mpango Wa Kwenda Kufanya Kazi Zake Nje Ya Nchi Tena

Mwanamuziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee anayefanya vizuri kwa hivi sasa na kibao chake cha ‘Wet’ amefunguka na kusema kuwa hana mpango wa kwenda nje ya nchi kutengeneza video kwani hapa Bongo kuna madirector wakali.

Vanessa Mdee amefunguka na kudai kuwa kutokana na maprodyuza wa video za muziki kujitambua na kuanza kutengeneza kazi nzuri, hakuna haja ya kutoka nje kwa sasa.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Showbiz Xtra, Vanessa  ametambulisha  video yake ya wimbo namba tisa unaopatikana kwenye albamu yake hiyo uitwao Wet aliomshirikisha G Nako, aliongeza kwamba hata akiwa na hamu ya kufanya kazi na prodyuza wa nje atahakikisha anamleta Bongo ili ashirikiane na maprodyuza wa ndani kufanya kazi.

Kwa sasa kiukweli tutabanana hapahapa. Mambo ya kutoka nje huku maprodyuza wetu wanafanya kazi nzuri sioni kama ni kitu kizuri kwa sasa, binafsi kazi nyingi nitafanyia Bongo”.

Ni kawaida kwa mastaa wengi wa Bongo kama Diamond, Alikiba, Vanessa, Navy Kenzo kwenda kutengeneza video zao nchi za nje kama South Africa ambazo wamedai kuna madirector wazuri kabisa wa video lakini hivi sasa tunajivunia na vya kwetu kama Vanessa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.